ISSRADHANS: HABARI .kitaifa.

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot
Showing posts with label HABARI .kitaifa.. Show all posts
Showing posts with label HABARI .kitaifa.. Show all posts

Wednesday, 13 December 2017

HASHIM RUN GWE AMJULIA HALI ,LISSU NAIROBI

December 13, 2017 0


 Image result for lisu na rungwe nairobi
INAPENDEZA SANAA NI  NI UUNGWANA ,…..
AMBAPO MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA),hapa nchini, Hashim Rungwe Spunda,ni miongoni mwa wana siaisa ambaye  amemtembelea na kumjulia hali mbunge wa Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu Hospitali Nairobi alikolazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, Mjini Dodoma.

Akiwa Nairobi, Rungwe ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea Urais Mwaka 2015, ametoa wito kwa Watanzania kuwa na moyo wa upendo huku akiliomba Jeshi la Polisi na vyombo vya Dola ,kufanya kazi yao kwa kila njia kuwapata  waliomshambulia Lissu.

Siku ya tukio, Lissu alikimbizwa katika hospitali hiyo baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Area D, Mjini Dodoma, Septemba 7 mwaka huu ambapo amefanyiwa upasuaji mara kadhaa na anaendelea na matibabu.

Read More

Tuesday, 5 December 2017

"Serikali yawabana wamiliki wa nyumba."

December 05, 2017 0


 Image result for lukuvi
NA ISSA RAMADHANI,
SERIKALI  imesema kuwa ni marufu kwa wamiliki wote wa nyumba nchini kuwalipisha wapangaji wao kodi ya mwaka mzima badala yake iwape fursa ya kulipa kodi hiyo kwa mwezi mmoja mmoja.
Related image
Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ufunguzi wa jengo la ofisi za makao makuu ya shirika La nyumba nchini (NHC).

Amesema kuwa ni wakati Sasa kwa wamiliki wa nyumba nchini kuwapa uhuru wapangaji wao kulipa kodi kwa mwezi mmoja mmoja ili kuweza kuwapatia unafuu.

“Ni wakati sasa wa kuwapa uhuru wapangaji kulipa kodi ya mwezi mmoja mmoja badala ya miezi sita au kumi na mbili kama ilivyokuwa mwanzo,”amesema Lukuvi

Hata hivyo, Lukuvi ametumia nafasi hiyo kuwaonya madalali wote kulipa kodi kwani wamekuwa wakifanya kazi na kuchukua 10% ya pato lakini hawalipi Kodi.
Read More

Friday, 24 November 2017

Tanroads yatoa sababu ya ubomoaji Barabara ya Morogoro

November 24, 2017 0




Dar es saaam,WAKALA  wa Barabara Tanzania (Tanroads) umesema kutofautiana kwa mita zinazotumika katika ubomoaji nyumba zilizoko kuanzia eneo la Ubungo na Kiluvya, kunatokana na Sheria ya Hifadhi ya Barabara ta Mwaka 1932 na mipango ya Serikali.


Tanroads imesema sheria hiyo inataja umbali tofauti wa hifadhi ya barabara katika baadhi ya maeneo na imeendelea kuwa mwongozo kwa Barabara ya Morogoro.

Nyumba zinazobomolewa kati ya Ubungo na Kimara ziko ndani ya mita 90 kutoka katikati ya barabara, wakati zilizobomolewa kutoka Kimara Stop Over hadi Kiluvya ziko ndani ya mita 121.9.

Akizungumza na Mwananchi jana, kaimu mkuu wa Idara ya Mipango Tanroads, mhandisi Elson Mwelanzi alisema tofauti hiyo inatokana na mipango ya Serikali.

“Katika sheria hii iliyoanza eneo la Faya hadi Ubungo ni mita 22.5, kutoka Ubungo hadi Kimara Mwisho ni mita 91.7 na kutoka Kimara Stop Over hadi Kiluvya ni mita 121.9 hayo ndiyo maeneo ya hifadhi ya barabara,” alisema Mwelanzi.

Alisema sababu ya Kimara Stop Over hadi Kiluvya kuwa na umbali wa mita 121.9 ni kutokana na mpango wa Serikali wa kuwa na hifadhi kubwa ya barabara.

“Hii sheria ilibadilishwa katika maeneo mengine mwaka 1967 na baadaye mwaka 2000, lakini katika hifadhi ya Barabara ya Morogoro haijawahi kubadilishwa. Sababu mojawapo ni kwamba hii ni barabara kuu hapa nchini,” alisema.

Alisema sheria hiyo ni nzuri kwa sababu inapunguza gharama za malipo kwa wakazi waliojenga ndani ya hifadhi.

“Ujenzi ndani ya hifadhi ya barabara unasababisha miradi kuwa na gharama nyingi si tu kwa ajili ya ujenzi, bali pia kulipa wakazi waliovamia maeneo,” alisema.

“Nakumbuka watu walilalamika na wakashauri sheria hii ibadilishwe, lakini mimi sishauri hii ibadilishwe ibaki kwa sababu watu hawatajenga ndani ya hifadhi ya barabara na miundombinu itapangwa vizuri,” alisema.   

Read More

Wednesday, 22 November 2017

Mwigulu Awakosoa Chadema Kuhusu Tundu Lissu

November 22, 2017 0
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi ,Dokta Mwigulu  Nchemba pichani

NA MWANDISHI WETU.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania, Dkt Mwigulu Nchemba amewakosoa upinzani kutumia tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kama ajenda katika kampeni za uchaguzi wa marudio na kusema kwamba chama hicho kimefilisika.

Akiwa Masasi katika kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa tiketi ya CCM, Dkt Nchemba amesema kwamba kitendo hicho cha Chadema kufanya kila mahali tukio la Lissu kama ndiyo ajenda atakwenda kuwaambia wakazi wa Singida wawaangalie vizuri watu hao.

"Mimi nitaenda kuwaambia wana Singida kwamba tuwaangalie vizuri hawa watu. Wao  ni mwenzao kwenye Chama sisi ni ndugu yetu na tunatoka sehemu moja. Inawezekanaje wawe wanafurahia tukio hilo? Kama kuna kitu walikuwa wanataka kitokee ili warushe maneno kwa serikali" amesema Dkt Nchemba.


Aidha akiendelea Nchemba amesema Chadema wanamuona kama Lissu mtaji ndiyo maana hata polisi walipomtaka dereva wake ili kuweza kumhoji wameamua kukaa naye huko.


Pamoja na hayo Nchemba amewata watu wakapige kura bila kuhofia fujo zinazoweza kufanywa na wanachadema kwani serikali ipo kwa ajili ya kusimamia sheria.
 "Wamezoea kufanya fujo. Nendeni mkapige kura akitokea mtu atakayethubutu kukughasi wewe mkariri sura alafu sisi tutamfundisha ustaarabu wa vyama vingi. Anayefanya fujo atakutana na mkono wa sheria. Na uzuri vijana wangu wapo hapa atakayethubutu kufanya fujo, Muwaonyeshe kwamba mmepitia mafunzo" Nchemba


Hata hivyo Nchemba amewataka wananchi hao kuichagua CCM kwa kazi nzuri inayofanya na kuwaamba kuuchagua upinzani wakitegemea itashinda ni sawa na kujeruhi nafsi.



Read More

Msajili wa Vyama vya Siasa apelekwa Mahakamani na Chama cha ‘Mtikila’

November 22, 2017 0

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi.  

NA YUSUPH MWAMBA,

CHAMA CHA DEMOCRATIC (DP), kimeomba kibali cha kumfungulia mashtaka msajili wa Vyama vya Siasa nchini. jijini Dar es salaam, Tanzania.

Chama hicho ambacho kiliasisiwa na Mchungaji Christopher Mtikila ambaye sasa ni marehemu kimewasilisha maombi Mahakama Kuu, kikiomba kibali cha kumfungulia kesi msajili wa Vyama vya Siasa kikimtuhumu pamoja na mambo mengine kuingilia mambo yake ya ndani.

Maombi hayo yaliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dar es Salaam dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) yamepangwa kusikilizwa na Jaji Kiongozi, Ferdinand Wambali, Jumatatu ijayo.

Kwa mujibu wa hati ya maombi ya faragha yaliyowasilishwa mahakamani hapo chama hicho kimefikia uamuzi huo baada ya msajili kukiandikia barua mbalimbali ikiwemo ya kubatilisha mkutano mkuu wa chama uliofanyika Mei 26.

Pia, chama hicho kinapinga hatua ya msajili kutowatambua viongozi wa chama hicho waliochaguliwa katika mkutano huo na badala yake kuwatambua wasio viongozi na wasio wanachama.


Read More

TANESCO wapewa onyo na Serikali

November 22, 2017 0



NAIBU  waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa Tanesco kuha kikisha kuwa hawakati Umeme bila sababu maalum na hivyo kuwaondolea wananchi adha ya kukosa nishati hiyo.

Naibu Waziri aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa TEDAP unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za Umeme ambapo vituo vya kupozea Umeme alivyovitembelea ni Mbagala, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre.

Naibu waziri wa nishati,Subira Mgulu (katikati),akitoa maelezo kwa Kaimu wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme.


“Umeme ukatike pale inapostahili tu, na endapo tatizo linatokea mfano kwenye mifumo ya Umeme ni muhimu mkatoa taarifa mapema kwa wananchi,” alisema Subira Mgalu.

Aliongeza kuwa ukatikaji wa Umeme unasababisha malalamiko kutoka kwa Wananchi kwani kukosekana kwa nishati hiyo kunaathiri shughuli nyingi hasa za kimaendeleo na kiuchumi zinazowaingizia kipato.

Aidha Naibu Waziri aliwaagiza watendaji wa TANESCO wanaosimamia mradi huo wa TEDAP jijini Dar es Salaam, kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika tarehe 15 Desemba, 2017.

Vilevile alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwake kutaboresha hali ya upatikanaji wa Umeme katika jiji la Dar es Salaam.

“Nawaomba watanzania wawe na matumaini na Serikali ya Awamu ya Tano kwani inajitahidi katika Ujenzi wa miundombinu ya Umeme, nia ikiwa ni nishati ya Umeme kupatikana muda wote,” alisema Naibu Waziri.

kwa upande wake, Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manirabona alisema kuwa Shirika hilo linafanya juhudi mbalimbali ili utekelezaji wa mradi huo ukamilike ndani ya muda ulioelekezwa.

Mradi wa TEDAP unahusisha upanuzi na ujenzi wa Vituo Vipya 19 vya kupoza Umeme wa Msongo wa kV 132/33 na kV 33/11 pamoja na ujenzi wa njia za Umeme wenye Msongo wa kV 132, kV 33 na kV 11 katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Kilimanjaro.

Gharama za utekelezaji wa mradi husika ni Dola za Marekani milioni 43, ambazo zimetolewa na Benki ya Dunia (WB) kupitia Mradi huo.




Read More

Friday, 27 October 2017

Waziri Kigwangalla atoa agizo la marufuku

October 27, 2017 0


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Maliasili na Utalii hapa nchini Dkt. Hamisi Kigwangalla  ameagiza kusitishwa mara moja  kwa oparesheni ya kukamata mifugo katika pori Tengefu la Loliondo na kuagiza mifugo iliyokamatwa kuachiwa mara moja.  

Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla kushoto akizungumza.


Aidha pia Kigwangala amesema hayo leo na kusema mifugo mbalimbali ambayo imekamatwa na bado kufikisha mahakamani iachiwe bila masharti yoyote na wafugaji waendelea kutumia vyanzo vya maji ndani ya pori hilo. 

Pia Waziri Kigwangalla anasema maamuzi hayo aliyofanya ni hatua ambayo inalenga kutoa nafasi ya kushughulikia mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo.


Oktoba 19, 2017 Waziri Kigwangalla alitoa agizo kuwa mifugo na matrekta ambayo yapo kwenye pori hilo Tengefu la Loliondo viwe vimeondoshwa na kusema baada ya siku 7 mifugo na mali za watu hao vingekutwa kwenye pori hilo basi Serikali ingevitaifisha.



Read More

Post Top Ad

Your Ad Spot