INAPENDEZA SANAA NI NI UUNGWANA ,…..
AMBAPO MWENYEKITI
wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA),hapa nchini, Hashim Rungwe Spunda,ni
miongoni mwa wana siaisa ambaye amemtembelea na kumjulia hali mbunge wa
Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu Hospitali Nairobi alikolazwa baada ya
kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, Mjini Dodoma.
Akiwa Nairobi, Rungwe ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea Urais Mwaka 2015,
ametoa wito kwa Watanzania kuwa na moyo wa upendo huku akiliomba Jeshi la
Polisi na vyombo vya Dola ,kufanya kazi yao kwa kila njia kuwapata waliomshambulia Lissu.
Siku ya tukio, Lissu alikimbizwa
katika hospitali hiyo baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu
wasiojulikana nyumbani kwake, Area D, Mjini Dodoma, Septemba 7 mwaka huu ambapo
amefanyiwa upasuaji mara kadhaa na anaendelea na matibabu.
No comments:
Post a Comment