![]() |
Miriam Jolwa maaru ‘Jini Kabula’ |
NA YUSUPH MWAMBA
MSANII
mwenye uwezo mkubwa na ubunifu nchini, kwenye tasnia ya Bongo Muvi kutoka
Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa maarufu kama ‘Jini Kabula’ amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuiigiza badala
yake anajiwekeza kwenye ujasiriamali.
Kabula,ambaye hivi karibuni alizua taharuki baada ya
kupatwa ugonjwa ambapo kwa sasa hali yake inakwenda vizuri na afya yake
imeimarika.
Akizungumza na mwandishi Kabula, alisema sio kwamba
ameachana na sanaa moja kwa moja lakini ameona akae pembeni ili kuangalia upepo
mwingine ambako kwa sasa amejielekeza kwenye masuala ya ujasiriamali.
“Nipo poa kwa sasa namshukuru Mungu , afya yangu
imeimarika, kikubwa kwa sasa nipo nje ya sanaa, lakini sijaiacha kabisa nafanya
biashara zangu upepo ukikaa sawa nitarudi ila najua hakuna atakaechukua nafasi
yangu kwakuwa kabula ni mbunifu na mtu makini katika kazi zake”, alisema
Msanii huyo, aliyewahi kutamba kupitia Tamthilia
ya Jumba la Dhahabu , yupo mbioni
kuzindua nembo ya biashara zake
anazoziendesha japo hakutaka kuziweka
hadharani.
No comments:
Post a Comment