Makubwa ya mzambarau: magome, mizizi, matunda - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday 11 December 2017

Makubwa ya mzambarau: magome, mizizi, matunda



 Image result for zambarau
·      Hutibu, tezi dume, saratani, bawasiri
·      Vijana kuwa rijali,  usichana waliokoma hedhi

NA ODRIANI NICOLAUS
WATU wengi mjini na vijijini hupenda kupanda mti wa mzambarau kutokana na mti huo kuwa na kivuli kizuri; ingawa kutokana na ongezeko la hitaji la mbao kila uchao wengine  hupanda mti huo kwasababu hiyo.

Kwasababu  ya kutofahamika sana kama mti dawa (medicinal plant) ndiyo maana mzambarau hauvumi kwa sifa,  japokuwa ni mti muhimu kiafya kutokana na dawa zilizomo kwenye mti huo, kwa mujibu wa maelezo ya wataalamu wa afya.
Dk. Elifariji Mtango, mtaalamu nguli wa sayansi ya mimea kutoka hopitali ya Chuo Kikuu cha  Kimataifa ya Tiba na Afya (IMTU) cha Jijini Dar es Salaam, anasema majaribio ya tiba kwa wagonjwa kadhaa yanaonyesha kuwa mizizi, magome na matunda ya mti huo husaidia tiba, kinga na lishe muhimu kwa afya ya binadamu.

Anasema Matunda ya mzambarau (zambarau) yana virutubisho vilivyomo kwenye mbegu za tunda  vinavyosaidia  kuweka katika uzani sawa kiwango cha sukari  mwilini. Wakati magome hutibu saratani za aina mbalimbali na tezi dume kwa  mizizi.

Akifafanua kuhusu mizizi, Dk.Mtango anasema kama ilivyo tezi dume,  mizizi ya mti huo iliyochimbwa, kusafishwa na kukaushwa juani kisha kuchemshwa vizuri pia hutibu matatizo ya hedhi kwa wanawake waliokoma hedhi kabla ya  umri sahihi wa ukomo.

Kama haitoshi, maji hayo huongeza kinga mwili na nguvu za kiume kwa vijana na na watu wanaume wengine wenye tatizo la kupungua  nguvu za kiume, na tatizo la kuota kinyama katika sehemu ya haja kubwa (bawasiri).

“Wapo watu waliowapa  tiba kwa mti huu na  kupata matokeo mazuri, kutoka kwenye mateso makubwa na sasa ni wenye furaha. Wanaendelea kufanya kazi zao bila matatizo yoyote ikiwamo kurejesha heshima kwa ndoa ambazo zilikuwa mashakani kutokana tatizo la nguvu za kiume, kuwaondoa katika gharama za tiba  sukari na presha ambayo yamekuwa tatizo kwa kizazi cha leo,”alisema.

Naye mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho vya asili wa kituo cha Mandai Herbal Clinick, Abdallah Mandai anasema kisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya mfumo wa uyeyushwaji wa chakula ndani ya mwili. Ukosefu au upungufu wa kemikali inayoitwa insulin husababisha ongezeko la kisukari inayojionesha kwa kiwango kikubwa katika mkojo wa mwathirika.

Hata hivyo  jamii inatakiwa kufahamu kuwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari hayalengi katika kuuponyesha ugonjwa, ila kumsaidia mgonjwa aweze kuishi maisha ya kwaida.

Matumizi ya zambarau huweza kumpa ahueni mgonjwa wa kisukari na kufafanua kuwa  kinachopaswa kufanyika ni kukausha mbegu za zambarau, kisha  kusaga mbegu hizo ili kupata unga laini.

Baada ya kufanya hivyo tumia nusu kijiko cha chai cha unga huo wa zambarau katika nusu glasi ya maji kila siku asubuhi kabla ya kula chakula chochote.
“Unaweza pia kuchemsha majani mabishi (yale laini) na magome mabichi haya humkinga mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa sukari hasa kwa wale ambao wameanzwa na dalili…  huweza kujikinga kwa kunywa glasi moja yenye miligramu 200 hadi 350  na kunywa ujazo huo asubuhi kabla ya kula kituo chochote na jioni kadri utakavyoshauriwa na mtaalamu,”alisema.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, juice hiyo husaidia mzunguko wa damu mwilini kutokana na uwepo wa dawa katika majani hayo. Hiyo ni pampoja na dawa hizo kusafisha taka kwenye mapafu ili kuruhusu oksijeni kupita vizuri na mtu kupumua ipasavyo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot