Elimu ya Shule ya Msingi Kuwa Miaka Sita - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, 10 November 2017

Elimu ya Shule ya Msingi Kuwa Miaka Sita




NA ISSA RAMADHANI.

SERIKALI  inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa elimu hapa nchini ambao elimu ya msingi itakuwa inatolewa kwa miaka 6,  tofauti na ilivyo sasa  ambapo hutolewa kwa miaka 7.
Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda Akiwa Bungeni.

Akijibu swali linalohusu,watoto wa kike kuolewa wakiwa na cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari, Naibu Waziri wa TAMISEMI  Mheshimiwa  Joseph  Kakunda ametolea ufafanuzi  suala  hilo  Bungeni  hivi karibuni mjini Dodoma na  kusema  “ mfumo huo mpya utatoa fursa kwa wanafunzi wa elimu ya msingi kusoma miaka 6, huku chekechea ukiwa ni mwaka mmoja na sekondari ni maka minne, ambayo itakuwa ni lazima”. Alisema
Wanafunzi wa shule ya msingi

Akifafanua  pia “Napenda kutoa majibu sahihi waliopata  mkanganyiko, nilisema sera mpya ya elimu huko tunakoelekea inabadilisha mfuo wa sasa wa elimu ambao utahitaji mtoto aanze chekechea mwaka mmoja, elimu ya msingi miaka 6, sekondari miaka minne  na  itakuwa ni lazima”, Alisema  Mheshimiwa Kakunda.

Aidha Mheshimiwa  Kakunda  ameendelea   kueleza  kutokana  na mfumo  huo  mpya  ambao  utaruhusu  mwanafunzi  kusoma kwa  muda  mfupi, na  baada ya kuhitimu  ndio  utakuwa  kithibitisho  pekee  kwamba  binti  amemaliza elimu ya sekondari na ndipo ataruhusiwa  kuolewa.

Hivi  karibuni  Waziri kakunda alitoa  taarifa  ikisema  kwamba  ili  mtoto wa  kike aweze kuolewa atahitaji kuwa na cheti cha kuhitimu sekondari, suala ambalo liliibua mjadala kwa wananchi.

NEWS FROM TANZANIA.



   

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot