yanga wakiwa mzoezini
WAKATI
zimebaki siku nne tu kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Desemba
15,nchini Kocha wa Yanga, George Lwandamina leo Jumatatu anatarajia
kupokea jina la mshambuliaji raia wa DR Congo kutoka kwa mwenyekiti wa usajili
wa timu hiyo, Hussein Nyika, ambaye
alikuwa nje ya mipaka ya Tanzania, kwa ajili ya kusaka mshambuliaji.
Ambapo Nyika alitembelea nchi ya Ghana,
Congo na Burundi lengo ni kutafuta mshambuliaji wa kimataifa ambaye atajiunga
na timu hiyo kwa ajili ya kuongeza nguvu kutokana na washambuliaji wa
kutumainiwa Amissi Tambwe na Donald Ngoma kuwa majeruhi jambo ambalo limesababisha kuwategemea Ibrahim Ajibu na Mzambia, Obrey Chirwa pekee.
Hata hivyo ,Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu Yanga kimesema kuwa
Nyika anatarajiwa kukutana na Lwandamina kwa ajili ya kumpa ripoti juu ya aina
gani ya mshambuliaji ambaye anaweza kujiunga na timu hiyo baada ya kufanya
uchunguzi kwenye nchi za Congo, Ghana na Burundi ambapo alienda kwa lengo la
kusaka mshambuliaji.
Kocha wa Yanga, George Lwandamina |
“Leo Jumatatu, mwenyekiti wetu wa usajili,
Hussein Nyika anatarajia kufanya kikao na kocha, Lwandamina kwa ajili ya kumpa
mrejesho wa kile ambacho amekutana nacho baada ya kwenda nje kusaka mshambuliaji
ambaye kocha anamuhitaji kabla ya dirisha kufungwa.ili kuendelea kwa
ligi kuu Tanzania bara “VPL”
“Hadi sasa kuna majina ya washambuliaji
watatu kutoka nchi za DR Congo, Ghana na Burundi ambapo alienda wiki chache
zilizopita kwa ajili ya kuangalia ni nani ambaye anaweza kuwa msaada katika
kipindi hiki ambacho fowadi yetu imepungua makali kutokana na baadhi yao kuwa
majeruhi,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, alipotafutwa Nyika ili aweze
kuzungumzia hilo, hakuweza kupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu
bila ya kupokelewa.
No comments:
Post a Comment