Theresia Mmbando |
NA
ISSA RAMADHANI.
SHIRIKA
la Kuhudumia Viwanda vidogo (SIDO) nchini ,kuongeza kasi ya utoaji mafunzo kwa
wajasiriamali na limetakiwa kuwaandaa kuanzisha viwanda vidogo, ambavyo vina
mchango katika ukuaji wa uchumi.
Akifunga kuhusiana na mafunzo ya ujasirialimali ,kuhusu usindikaji, uhifadhi wa chakula na ufungashaji juzi, katibu tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando alisema mafunzo hayo yatahamasisha wajasiriamali kuanzisha viwanda.
Mmbando alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yanalenga kuwapatia ujuzi wa kutumia malighafi zinazopatikana nchin na kuzalisha bidhaa ambazo zitatumiwa na Watanzania.
“Sido ongezeni kasi ya mafunzo haya kwani viwanda vidogo vitapunguza upotevu wa mazao usio wa lazima,” alisema.
Naye meneja wa Sido wa mkoa huo, MackDonald Maganga alisema mafunzo hayo yalikuwa kwa ajili ya wakufunzi wa ujasiriamali (Tot) kutoka mikoa ya Tanga, Njombe, Shinyanga, Singida na Dar es Salaam.
Maganga alisema baada ya kupata mafunzo watakwenda kuelimisha wenzao.
Alisema mbali na mafunzo hayo, pia kulikuwa na mafunzo ya usindikaji wa vyakula na uhifadhi wa vyakula ambayo yatawasaidia wajasiriamali hao kuanzisha viwanda vidogo.
Alisema shirika hilo litaendelea kutoa mafunzo ili kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda ili kuwa nchi ya uchumi wa kati.
“Ninawashauri wajasiriamali waendelee kufika Sido kila wanapohitaji ushauri kuhusu biashara zao,”alisema.

No comments:
Post a Comment