NA
GEORGE MSHANA
DAWATI linaloshughulikia mikopo kwa wateja wanaoishi
na Virusi vya Ukimwi (VVU) la Benki ya Mkombozi (Mkombozi Bank) limewashauri
watu wanaoishi na Virusi vya Ugongwa wa Ukimwi kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba
kwa kufungua akauti ili kuwa sifa ya kupata mkopo badala ya baadhi yao kukata
tamaa.
Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Benki hiyo, Rose Mpeleta pia aliwashauri kujiunga kwenye
vikundi ili kuungwanishwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kupitia mfumo huo
waweze kupata matibabu kwa kadi za mifuko hiyo au ya Bima ya Afya (NHIF).
Alisema
dawati hilo limeanzishwa mahususi kwa
kundi hilo kutoa mikopo ya riba
nafuu ingawa tathimini inaonesha kiwango
cha wanaopewa mikopo hakiridhishi ukilinganisha na hali halisi, hivyo kutoa ushauri kwa wahusika kuchangamkia fursa
hiyo.
“Kiasi
ambacho kila mteja kwenye kikundi anaweza kupata kinaanzia 300,000/-… mteja
anaweza kupata mkopo wa miezi mitatu hadi
tisa kwa riba ya asilimia 2.5 tu. Marejesho hufanyika baada ya miezi mitatu. Mteja
anaweza kupata mkopo bila kuwa na dhamana isiyohamishika,” alisema Mpeleta.
Alisema
tofauti na benki zingine, mteja huandalia kabla kukopa ikiwa ni pamoja na kufundishwa
katika madarasa maalimu mbinu mbalimbali za kibiashara kama vile kutunza
kumbukumbu za hesabu, sababu na umuhimu wa kukopa, kufungua akauti, nidhamu ya
mkopo, umuhimu wa marejesho na madhara ya kukopa na kutorejesha.
Kwa kutumia mfumo huo alisema wafanyabiashara
na wajasiriamali wadogo na wakati wanaofanya biashara katika mfumo rasmi na
usiokuwa rasmi wameweza kukopa na kuendesha biashara zao na kurejesha bila
kusuasua.
Hiyo
pia ni mikopo hiyo kutolewa kwa masharti nafuu kama vile riba ndogo na benki
hiyo kutokuwa na sharti gumu la dhamana isiyohamishika kama vile nyumba.
“Lengo letu ni kuwakwamua watu kiuchumi kwa asilimia 100,” alisema.
No comments:
Post a Comment