`Hakuna nembo ya TBS bila Barcode ya Tanzania’ - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, 11 December 2017

`Hakuna nembo ya TBS bila Barcode ya Tanzania’



NA GEORGE MSHANA


  Image result for tbs tanzania

WAFANYABIASHARA hapa nchini wameshauriwa kuwa alama kuthaminisha biadhaa (Barcode)  ili kuzifanya bidhaa zao kuuzwa katika masoko makubwa ya ndani na nje ya nchi. 
 
Ili kufikia malengo Taifa la Uchumi wa Kati kwa njia ya biashara na viwanda.
Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam na Afisa Masoko wa Kampuni ya Global Standard 1 (GS1 Tanzania) Musa Fundi katika mahojiano maalumu na gazeti hili na kufafanua kuwa baadhi ya wafanyabishara hushindwa kufikia ndoto za kibiashara kwa kutojua umuhimu wa nembo hiyo na ya Shirika la Viwango (TBS) katika kuongeza wateja.

 “Wafanyabiashara wengi hawana mtazamo kuuza bidhaa zao ngazi ya kimataifa…wakati mwingine ni kwa kutojua mbinu za kufika huko. Hata baadhi ya nembo muhimu kama barcode hawajui umuhimu wake...tumeanza kutoa mafunzo haya kwa kushirikianana Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO),”alisema Fundi.

Alisema pia GS 1 wameanza kuelekeza wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo namna bora ya kufungasha bidhaa, umuhimu wa nembo zinazoonesha nembo ya ubora, mwisho wa matumizi  ya bidhaa kwani   mambo hayo ni muhimu kwenye bidhaa hasa katika soko la kimataifa.

Afisa Masoko huyo aliongeza kwa kusema kuwa shirika lake limeingia makubaliano na Shirika la Viwango (TBS)  kuhamasisha wafanyabiashata kuwa na Barcode kabla ya kuomba kusajili upya alama ya TBS katika bidhaa husika.

“Ni agizo la  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kufuatia barua ya waziri mwenye dhamana nkuwashauri wajasiriamali watumie barcode ya Tanzania. Hii itasaidia mnunuzi ajue kuwa hiyo bidhaa imetoka na imetengenezwa Tanzania,”alisema.  

Alisema bidhaa nyingi za hapa nchini zimewekwa nembo hiyo kutoka  Kenya  na  Afrika Kusiwakati ukweli ni kwamba  imezalishwa Tanzania. Hivyo kwa sasa lazima kila  bidhaa ijulikane imetengenezwa Tanzania, lazima iwe na barcode ya Tanzania, alisisitiza.

Fundi alisema kupitia  serikali za mitaa mbalimbali, jumla ya wajasiriamali 19,800 wanatarajiwa kupatiwa nembo ya Barcode kufikia mwishoni mwa mwaka. Hadi  sasa 16,800 wamekwishapatiwa.
“Tunaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu huu, ambapo wengi wamebadilika na baada ya kuina mafanikio kwa wengine,”alisema.

GS1 Tanzania ilianzishwa kwa malengo ya kutoa bar code kwa wajasiriamali ambao  wanazalisha bidhaa mbalimbali. Bar code inayowekwa kwenye bidhaa zao, inawasaidia bidhaa hizo ziweze kuuzwa kwenye masoko makubwa na kwenye masoko ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot