
KLABU ya Yanga imeshindwa kumpa kiungo Mohamed
Ibrahim ‘Mo Ibra’ kile anachotaka, hivyo leo Jumatatu mchezaji huyo anatarajiwa
kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu yake ya Simba.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa Mo,
Jamal Kisongo amesema kuwa mteja wake huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka
miwili na Simba baada ya kushindwana na Yanga ambao nao walikuwa wanamtaka
huku Msimbazi wao wakitimiza makubaliano waliyokuwa wanataka.
Alisema walifanya mazungumzo na Yanga
lakini kuna baadhi ya vitu kwenye mkataba hawakuridhika navyo na walipozungumza
na Simba wakakubali kurekebisha baadhi ya vipengele kwenye ule mkataba wa awali
hivyo rasmi mteja wake anabaki Simba na leo atasaini kandarasi baada ya ile ya
awali kumalizika.
“leo natarajiwa kwenda kusaini mkataba
mpya wa miaka mawili na mchezaji Mohammed pale Simba baada ya ule wa awali
kumalizika, hivyo tunaongeza mwingine.
“Yanga nao walionyesha kumhitaji lakini
kuna vitu walishindwa kukamilisha na tulipozungumza na Simba wamekubali
kurekebisha baadhi ya vipengele, hivyo atabaki huko,” alisema Kisongo.
No comments:
Post a Comment