NA AHMED
MAKONGO, BUNDA
Mkurugezi wa halmashauri ya mji wa Bunda, Janeth Mayanja akifafanua jambo(pichani) |
WAZAZI na watu wengine
wa kijiji cha Migungani Kata ya Bunda Stoo, mkoani Mara wameungana kujenga
shule ya sekondari karibu na makazi yao ili kuwanusuru kuliwa na wanyama wakali
wanafunzi wanaoishi mbali na shule.
Wakizungumza
na gazeti hili, baadhi ya wazazi walisema ili kutumiza mpango huo wamekubaliana
kuchangishana kiasi Shilingi 121,000 kila kaya.
Walisema
Kata ya Bunda Stoo ni kati zilizoko karibu na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
JamboIlielezwa
kuwa mkuu wa wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, ndiye aliyehamaisha ujenzi huo
na kuelekeza eneo la ujenzi.
“Nami nawahamasisha kila mmoja kuwekeza kwenye
elimu badala ya mambo mengine ambayo hayana manufaa kwa maisha ya baadaye ya
watoto wenu,”alisema wakati alipotembelea kijijini hapo.
Mkurugezi
wa halmashauri ya mji wa Bunda, Janeth Mayanja, alisema kuwa kutokuwepo kwa
sekondari katika kata hiyo ni changamoto kubwa na kuwataka wananchi, wakiwamo
wafugaji katika eneo hilo kuendelea kuchangia nguvu zao kufanikisha ujenzi huo
haraka ili ikiwezekana masoko yaanze mwakani.
Nao baadhi ya wananchi wa kata hiyo walielezea
furaha yao kutokana na kuanza kwa ujenzi wa sekondari hiyo, wakisema kuwa
watoto wao wametaabika kwa kipindi kirefu kwa kutembea umbali mrefu, huku
wakikumbana na changamoto ya kushambuliwa na wanayama wakali.
No comments:
Post a Comment