Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mkoa wa Pwani, Mhandisi Mshamu Munde akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mwandege, |
NA YUSUPH
MWAMBA, MKURANGA
MGOGORO kati ya mwekezaji,
Kampuni ya Azam na baadhi ya Wananchi wa
Kijiji cha Mwandege, Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani huenda
ukafikia kikomo baada ya halmashauri hiyo kumaliza uandikishaji wa Wananchi
wanaodai fidia dhidi ya mwekezaji huyo.
Akizungumza
na Raia Tanzania, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa
Pwani, Mhandisi Mshamu Munde, alisema hatua iliyoba ni kukabidhi ripoti ya mapendekezo kati ya pande
mbili , Baraza la Taifa la Usimamizi naUhifadhi wa Mazingira (NEMC) na
Halmashauri kwenda Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira iliyotaka
ripoti hiyo.
Akifafanua,
Mkurugenzi huyo aliwataka Wanakijiji hao kuwa wavumilivu wakati huu serikali
ikikamilisha taratibu zilizoshauriwa na kuwahakikishia kuwa kila anayestahili
atapewa haki yake.
Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina akitaja sababu. |
Hata
hivyo alikiri kuchelewa kwa taarifa hiyo nje ya muda wa siku 14 zilizotolewa na
aliyekuwa Naibu Waziri wa Mazingira na
Muungano, Luhaga Mpina akitaja sababu mbalimbali ukiwamo uchunguzi wa kina kuhusiana na
mgogoro wenyewe kuchukua muda mrefu.
Sababu
nyingine ni kubaini kiini cha mgogoro ambapo katika uchunguzi huo ilibainika
kuwa malalamiko yamegawanyika, wanakijiji kadhaa wanamlalamikia mwekezaji huyo
kutiririsha maji yenye viambata vya kemikali kwenye maeneo yao, kelele na
harufu mbaya.
Wakati
wengine wanadai nyumba zao zao kumoboka
kutokana na maji yanayotiririka kutoka kiwandani humo, alisema.
Mmoja
wa wanakijiji hao, Said Mkawala alisema wanaishi kwenye eneo hilo kwa miongo
kadhaa ingawa mwaka 2009 Kampuni ya Azam
ilijenga kiwanda karibu na makazi yao kabla ya kuanza uzalishaji mwaka 2010 na
kutokea kwa madhara hayo.
“Naibu waziri wa Mazingira alikuja hapa Oktoba 2017 baada ya kusikia kero zetu
za muda mrefu , akakutana na mwekezaji baada ya kutoka maagizo yaliyowafikia
viongozi wetu ni kwamba ndani ya siku 14 kuwe na maafikiano ili suluhisho
lipatikane, lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea. Ikumbukwe tumesimamishwa
kufanya shughuli zetu hadi muafa wa suala hili, sisi tupo tayari kulipwa fidia
na kuondoka kuliko hali hii,”alisema akiwakilisha wenzake 39.
Kwa
mujibu kifungu 57 (b) (i) cha sheria ya Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 hairuhusiwi kujenga mradi wowote ndani ya
mita 200 kutoka makazi ya watu bila ruhusa maalumu , tathimini ya mazingira
(EIA) kufuatwa.
Hata
hivyo Mkurenzi, Munde alisema taratibu zote za mazingira zilizingatiwa wakati
wa ujenzi wa kiwanda hicho mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment