Jinsi ya Kufanya Mazoezi Nyumbani - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, 8 November 2017

Jinsi ya Kufanya Mazoezi Nyumbani

NA ISSA RAMADHANI.
MAZOEZI  ni muhmu kwa binadamu wote si lazima uwe mgonjwa na upewe ushauri wa kitabibu ndo unaanza kufanya mazoezi.  Hata hivyo sio kila mtu anayependa kufanya mazoezi gym. Kwa kulipia katika chumba maalumu cha kufanya mazoezi ya viungo na mengineyo kwa utaratibu maalum na kusimamiwa ili kuwa na afya njema. 

sit up
Aidha wengine tunapenda kufanya mazoezi nyumbani kwa sababu moja au nyingine.hasa kuwa na muda mdogo nikitoka kazini.Wataalamu wanashauri kufanya mazoezi husaidia mwili kuwa na ufanisi mzuri wa kzi na ukuaji wa mwili na akili.Ila siyo lazima kufanya mazoezi sehemu za kulipi hat nyumbani unaweza fanya.  
Fuata hatua za kufuata  5 za kufanya mazoezi nyumbani:
1. Andaa eneo maalum / iwe chumba.
Utahitaji nafasi maalum kufanya mazoezi, ili uweze kuyafanya bila shida na kwa hiyo, hakikisha chumba au eneo lina nafasi isiyopungua futi 5 kwa futi 5 na pan hewa ya kutosha na mwanga. Pia uwe na kapeti nzuri kwa ajili ya zoezi la kulala chini.
2. Tumia chochote kile!
Iwe kamba au ukuta, ngazi, viti, hata kikapu cha nguo chafu! Unaweza ukatumia vifaa hivi kwa mazoezi. Kwa mfano:
·         Panda na kushuka kwenye ngazi mara nyingi
·         Beba fagio kwa usawa ukiwa una ruka kichurachura
·         Shika ukuta alafu ruka kichurachura na kamba pia ni muhimu.
3. Vifaa muhimu
Utahitaji vifaa vya kufanya mazoezi kama vifaa vya kupiga chuma, kamba na mengineyo.
4. Jifunze mazoezi ya kawaida
Kwa kuwa utakuwa unafanya mazoezi nyumbani kwako , mazoezi ya kawaida ndio yatakusaidia sana, mfano:
·         Sit up
·         Push up
·         Kuruka kichurachura
·         Step up
·         Crunches


Haya ni mazoezi ya kawaida, lakini kila moja ina jinsi nyingi kiafya za kuifanya. Kwa maelezo zaidi juu ya hii, soma yafuatayo kutoka Greatist.
5. Mashine za mazoezi
Kuwa na role up au treadmill (mashine ya kukimbia), baisikeli ya mazoezi na mengineyo yanaweza kukupa motisha zaidi kufanya mazoezi. Ukiwa nayo, kuna uwezekano mkubwa wa kwamba utaitumia. Anza sasa tafuta mashine za mazoezi zinauzwa kwa bei nafuu madukani.
Anza
Kwenya swala la mazoezi, kuanza ndio ngumu zaidi vitu vyote vingine. Kwa hiyo, usifikirie sana. Amka kesho asubuhi alafu fanya mazoezi ya kawaida kwa dakika 30. Na edelea hivyo kidogo kidogokwa wiki mara 3. Kwa kufanya hivyo kwani mazoezi ni tiba ya maridhawa kiafya.
Na ushuri wangu kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku , mbali na ubize tuliono katika utafutaji .


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot