ABROMOVICH KUCHUNGUZA MAHUSIANO YA CONTE NA WACHEZAJI. - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, 8 November 2017

ABROMOVICH KUCHUNGUZA MAHUSIANO YA CONTE NA WACHEZAJI.



LONDON,CHELSEA.
MMILIKI  wa klabu ya Chelsea, Mrusi Roman Abramovich ameanza kuafanya uchunguzi wa kinachoendelea katika mahusiano ya kocha Mtaliano Antonio Conte na beki Mbrazil, David Luiz ni kufuatia kujiuzulu kwa Mkurugenzi wa Ufundi, Mnigeria Michael Emenalo juzi.
Roman Abramovich ni mmiliki wa Chelsea Fc

 Kwakuwa  Conte anadaiwa kumuweka benchi beki mkabaki Luiz kwenye  mchezo uliopita The Blues  wakishinda 1-0 dhidi ya Manchester United  na kwa kuhoji mambo fulani fulani ya kiufundi  mazoezini  kuelekea kwenye  mechi hiyo ya Ligi Kuu ya England.

Na hii ni kufuatia hali ya wasiwasi inayoibuka juu ya tabia yake Antonio Conte ya kugombana na wachezaji wake ndani ya Klabu yake, baada ya awali kuhitilafiana pia na Diego Costa. Hali inayoelezwa kuwa  mbabe katika upangaji na kiufundi zaidi kuheshimiwa katika maamuzi yake.   

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot