NA MWANDISHI WETU.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya
kutoka lebo ya
muziki ya WCB Wasafi Tanzania, Mwajuma Abdul a.k.a Queen
Darleen ametoa video
ya wimbo wake mpya kabisa ameupa jina ‘Nitakufirisi’ chini ya mtayarishaji Producer Laizer Classic katika studio ya Wasafi Records.
Mwajuma Abdul a.k.a Queen Darleen |
Ikiwa ni kazi ya pili kutoka kwa Queen Darleen chini ya usimamizi wa WCB Wasafi, baada ya ‘Kijuso’
aliyoshirikiana na Ray Vanny. ‘Nitakufirisi’ imetimiza ahadi ya
Queen Darleen iyotoka katikati ya mwaka huu katika
mahojiano na Dizzim Online kuwa mwishoni mwa mwaka
huu ataanza kuachia kazi zake rasmi.
Hata hivyo Queen katika ngoma hii mpya ameuzungumzia mfumo wa hali ya kimahusano waakina dada(kwa kuuvaa uhusika) na wanaume wenye kuamini nguvu ya pesa katika kujiridhisha kimapenzi kwa kuwapa jibu kuwa kwa mwendo huo atawafirisi ‘Nitakufirisi’.
No comments:
Post a Comment