MBUNGE wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi
Kabwe amefunguka na kudai kwamba utekelezaji wa miradi kupitia serikali ya
awamu ya tano inaharibu uchumi wa nchi bila kujali maslahi ya Taifa na wananchi
wake.
Zitto ametoa hayo ya moyoni kupitia
ukurasa wake wa Facebook na kusema kwamba Mkataba ambao serikali ya awamu ya
tano imeingia na Uturuki katika ujenzi wa reli haujawazingatia Watanzania wenye
viwanda vya chuma ambacho ni kitu kinachohitajika katika mradi huo wamenyimwa
na badala yake wamekabidhiwa kampuni ya Uturuki.
MBUNGE wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe |
Mh. Zitto ameongeza kwamba Mkataba
ambao serikali umeingia na Waturuki hao hauwalazimishi kutumia malighafi za
nyumbani ingawa wameingia mkataba wa sh. Triliomi 7.
"Kwa masikitiko makubwa
nawaambia Watanzania kuwa Mkataba wa Ujenzi wa Reli waliyopewa kampuni ya
Uturuki haukuzingatia maslahi ya Taifa.... . Watanzania wenye viwanda vya
kuzalisha Chuma kitu kinachotakiwa kwenye sehemu ya mradi wamenyimwa kazi
hiyo na badala yake kampuni za Uturuki ndio wamepewa kazi hizo. Hata kokoto
wamepewa kampuni ya Uturuki. Watanzania watakuwa vibarua tu" . Zitto.
Ameongeza kwamba "Nahisi
Serikali itazame hii miradi mikubwa na kuifungamanisha na mkakati wetu wa
Viwanda ili kufikia malengo yetu na azma yetu ya kuondoa umasikini nchini
kwetu. Hii Serikali ya Awamu ya Tano inaharibu uchumi wetu. Inatekeleza miradi
bila kujali maslahi ya nchi yetu. haina maarifa ya kuendesha uchumi,"
Mbali na hayo Mh. Zitto amefafanua
kwamba kama nchi ingekuwa na mipango thabiti basi Tanzania ingekuwa wazalishaji
wakubwa wa Chuma na na hata uzalishaji wa chuma cha kujengea reli kwenye eneo
la Mashariki mwa Afrika na Maziwa Makuu.
"Nchi yetu ina chuma kingi sana
kule Mchuchuma na Liganga, na pia tuna makaa ya mawe ya kuchenjua chuma hiki
ili kupata chuma cha pua (steel). Mradi huu wa reli peke yake ungeweza
kuchochea maendeleo makubwa kwenye sekta ndogo ya migodi na viwanda vya Chuma.
Iwapo tungekuwa na mipango thabiti, ".
No comments:
Post a Comment