“UKAWA watoa neno kuhusu Serikali ya awamu ya tano” - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday 11 December 2017

“UKAWA watoa neno kuhusu Serikali ya awamu ya tano”




UMOJA wa katiba ya wananchi (UKAWA ) nchi umesema kuwa umejiridhisha kuwa Serikali ya awamu ya Tano sio serikali ambayo inafuata utawala bora,  kuzingatia haki za binadamu huku ikivunja katiba.

Akizungumza na  waandishi wa habari, Mwenyekiti mwenza wa Umoja huo,  Freeman Mbowe  amesema vipo viashiria vingi vinavyoonesha kuwa uongozi wa awamu ya Tano hauzingatii katiba ikiwemo kuzuia mikutano ya kisiasa Pamoja na kushambulia  kwa viongozi wa vyama vya upinzani.

" Serikali inabana wazi  kuzungumzia na kuikosoa,  hata nyinyi wandishi hampo Salama, ndio maana mwenzenu  Azory  mpaka sasa hajapatikana na serikali haijatoa tamko lolote" amesema Mbowe.

Aidha Mbowe pia alizungumzia uchaguzi mdogo wa madiwani ambapo  Kata  43 zilifanya uchaguzi huku CCM, ikishinda Kata 42 na Chadema walishinda moja.

Alisema viongozi  wao wakiwemo wabunge, madiwani na wagombea wa upinzani walikua wakikamatwa na kuwekwa ndani huku wasimamizi wao wakitolewa nje ya vyumba vya Kura jambo ambalo ni kinyume na katiba ya nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot