
JAMII imeshauriwa kula
vyakula vua asili ili kuepuka madhara yanayotokana na ulaji holela wa vyakula
vyenye viambata vya kemikali na kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ambayo hutumia gharama kubwa kujitibu.
Uhauri
huo ulitolewa na mjasiriamali na mzalishaji wa vyakula kwa mfumo wa asili wa
siku nyingi jijini Dar es Salaam, Yohana Sefue wakati akizungumza na gazeti
hili lililotaka kufahamu juhudi za wazalishaji wa bidhaa za vyakula katika kupunguza tatizo la magonjwa
yasiyokuwa ya kuambukiza ambayo sehemu kubwa husababishwa na ulaji wa vyakula
vyenye kemikali.
Alisema
wakati umefika sasa kwa Watanzania kubadili mfumo wa ulaji, kusikiliza na kutii
ushauri wa wataalamu na kusema kuwa ni jamii yenyewe inaweza kuamua namna ya
kula ingawa ni wajibu wa wataalamu kutoa
elimu kwao.
“Wakati
wote huwa naamini kwamba kila ulacho `ndio wewe’ kwa maana kwamba mtu mwenyewe
huamua ale nini kwa faida yake mwenyewe kiafya. Je, unapoamua ule nini, unatafakari nini sahihi
kula kulingana na maelekezo ya wataalamu,?”alihoji.
Alisema
magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza kama saratani, kisukari, shinikizo la damu,
utapia mlo mkali (savior malnutrition) na magonjwa mengine ya mfumo wa chakula
huweza kuzuilika ikiwa watu watakula kwa wingi vyakula vya asili
vinavyoelekezwa na wataalamu.
Sefue
vyakula hivyo yakiwamo matunda yalizalishwa kwa njia za asili vina sifa
nyingine ya kujenga akili, kukinga mwili dhidi ya maradhi na mfumo wa damu
mwiliki kufanya kazi ipasavyo.
Aliongeza
kwa kuishauri jamii kula vyakula vilivyotengeneza kwa unga wa nafaka vyakula
zisivyokobolewa kama vile mahindi, ngano, ulezi na soya. “Hakuna sababu ya kwua
na watoto wenye utapia mlo. Kuendelea kwa ugonjwa huo katika jamii, ni ishara
kwamba vyakula vinavyotengezwa havitumiki au kutumika kwa kusuasua,”alisema.
Alisifu
juhudi za serikali kusimamia masuala ya afya hapa nchini na kushauri mamlaka
kuendelea kutoa elimu zaidi kuhusu lishe bora ili kupunguza tatizo la magonjwa
yasiyokuwa ya kuambukiza.
Hiyo
ni pamoja na kupanua wigo wa kilimo cha mazao yanayotumika kutengeneza bidhaa
za asili ili kuwepo kwa mali ghafi ya kutosha kutengeneza vyakula hivyo. Pia
kuhamasisha viwanda kuzalisha vyakula hivyo ili kutosheleza katika matumizi.
Takwimu
za wataalamu zinaonyesha kuwa asilimia 10 ya Watanzania wanaugua ugonjwa wa
kisukari huku asilimia 20 wakisumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu
(presha).Pia takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 42 ya watoto chini ya miaka
mitano wamedumaa wakati asilimia 16 walipoteza maisha na 21 kuzaliwa wakiwa na
uzito wa chini.
No comments:
Post a Comment