![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0Ja3bAP06cjPZA7pBV13MlLbcQyJ0PSd-_8SkvWQO6D3XeO8rmkTI4KjNSRwQ6_M44pfVYtFgK5HgeCHk3vNrtyQ8zVYxpjO-8udeCNQ6J2Dcz67928PiG33JNuQSGDzq62e6UIbr2Hs/s640/SIMBA+NA+KOMBE+LA+ASFC+1.jpg)
NA HASSAN RASHID
MABINGWA
watetezi
wa Kombe la Shirikisho la TFF, klabu
ya soka ya Simba inatarajiwa kuzindua rasmi michuano hiyo kwa msimu wa 2017/18 itakapocheza
na Green Warriors Desemba 22.
Hii ni kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF raundi ya pili ya michuano hiyo itacheza kwa siku tano kuanzia Disemba 20 hadi 24. Michezo ya Desemba 20 mwaka huu itakutanisha timu za JKT Mlale na KMC, Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera.
Aidha ,Mechi zingine siku hiyo ni kati Ambassador na JKT Oljoro, Boma FC na Ndanda, Mvuvumwa na JKT Ruvu, Abajalo itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons wakati Milambo ya Tabora itacheza na Buseresere ya Geita.
Na Desemba 21, 2017 Mshikamano itacheza na Polisi Tanzania, Rhino ya Tabora na Alliance ya Mwanza, Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya Kwanza ya Mbeya, Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma, Ashanti na Friends Rangers za Dar es Salaam, Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.
![Image result for simba fc bingwa wa shirikisho](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCTCk8U6VefXjrM73GwIjHf9i88GlCtT8hdtJX6B0w0vFkTKexcnHTVTjlUeXEC6bEm_FYFuU2s8BtBMcRisKWOFtUfRavg0HJxf5cj0xID3kquZUqnAi_jidqFxgZ5ONFvgRG5ExT-JCy/s640/SIMBA.jpg)
Mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo Young Africans itacheza na Reha FC, Desemba 24, 2017 siku ambayo pia Burkina ya Morogoro itacheza na Lipuli ya Iringa, Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma, Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
No comments:
Post a Comment