SAIKOLOJIA
NA ISSA RAMADHANI
NI jambo la kumshukuru
Mungu kukutana tena katia safu hii ya saikolojia na mahusiano. Leo tutazungumzia
tatizo la msongo wa mawazo na namna ya kuondokana nalo.
Mara nyingi katika jamii au familia zetu tumekuwa
tukishuhudia watu wengi wakisumbuliwa na msongo wa mawazo kwa kujua au kutojua
na tatizo hili limekuwa lilikuwa kwa
kasi.
Tafiti zimeonesha tatizo la msongo wa mawazo
likizidi husababisha mtu kuugua ugonjwa wa akili na kuingia gharama kubwa
katika matibabu.
Hata hivyo zipo njia mbalimbali ambazo mtu
anayekumbana na hali hii anaweza kuzitumia ili kuondokana nalo.
KUZUNGUMZA
NA WATU
Wataalamu wa saikolojia wanasema kuzungumza na watu
ni njia mojawapo ya kuondoa tatizo la
msongo wa mawazo, Wanasema mtu anapoficha tatizo linalomsumbua mawazo
husongamana kwani yanakuwa yamekosa pakutokea hivyo kusababisha matatizo ya
kiafya hasa akili. Kiafya binadamu anapaswa kuongea na kusilizwa anapokumbana
na tatizo ambalo mwenyewe limemshinda kulitatua. Kwa kawaida mwanamke anapaswa
kuzungumza maneno 24000 na mwanamume maneno 6000 kwa siku ili aweze kuwa wa
kawaida.
KUWA
NA MUDA WA KUFURAHI
Kitendo cha kuwa na furaha hutibu tatizo la msongo
wa mawazo. Wataalamu wa saikolojia wanasema kucheka kunaongeza afya na siku za
kuishi, mfano nchi zilizoendelea kama Marekani
kuna maeneo maalumu yamejengwa watu wanaenda kuangalia vichekesho na kucheka
ili kuwaondolea msongo wa mawazo. Kwa ufupi kucheka na kufurahi ni tiba na ni
afya.
KUWA
NA MUDA WA KUTOA MACHOZI
Hili jambo wanasikolojia wanashauri unapopata muda
wa kulia fanya hivyo na usijizuie na inapobidi jiachie kulia hasa machozi
yatoke kwa wingi. Kwa bahati mbaya mila
za Kiafrika suala la kutoa machozi
inachukuliwa ni udhaifu au utoto kwa
mwanaume lakiniu katika sayansi kulia ni tiba. Wanasaikolojia wanasema machozi
yanasaidia kuondoa sumu mwilini na yanapotoka husaidia kuondoa bacteria na kufanya mtu kujisikia vizuri.
FANYA
KAZI UNAZOPENDA
Jitahidi kufanya jambo unalolipenda na kukupa
faraja, mfano kuangalia filamu, kuogelea, kusoma vitabu, kucheza mpira na mengineyo, hali hiyo
itakusaidia kuondokana na msongo wa mawazo..
JICHANGANYE
NA WATU
Ni vizuri ukajichanganya katika shughuli mbalimbali, mfano sherehe,
usafi, mikutano, mijadala, misiba na matamasha ya muziki. Huko utajikuta
ukizungumaza na kujadili mambo mbalimbali na kujifunza changamoto ambazo watu
wengine wanazipitia na kuondokana nazo.
KUWA
NA MUDA WA KUPUMZIKA
. Ukiwa nyumbani hakikisha unapata muda wa kutosha
kupumzisha mwili na kulala na hakikisha unakula vyakula vya kujenga mwilini na akili.
PENDEZESHA
CHUMBA UNACHO LALA
Si sebuleni pekee panatakiwa papendendeze bali na chumba unacholala kinapaswa kiwe safi, kuvutia kwa kupanga vitu vizuri na kuwa na hewa safi
ya kutosha Unapaswa kusafisha mashuka ya kitanda na kujifunika, godoro zuri,
kudeki chumba na kiwe na mwanga wa kutosha .
Wataalamu wa
masuala ya saikolojia na afya wanasema nusu ya maisha yako unatumia chumbani unakolala. Usiku lala kwa
muda usiopungua saa saba ili kuondokana na tatizo la msongo wa mawazo.
FANYA
MAZOEZI
Jitaidi kufanya mazoezi mara kwa mara angalau dakika
30 kila siku. Mazoezi si tu tiba ya msongo wa mawaz, bali pia hata kisukari na
moyo na kuboresha ufanisi wa mwilini.
SHUGULIKIA
TATIZO
Kama ukiona tatizo
haliondoki ni vyema ukawaona watu wa ushauri nasaha na wanasiaklojia ili kuona nama ya kuondokana na tatizo la msongo wa mawazo na mengineyo
No comments:
Post a Comment