Mahusiano'
NA
ISSA RAMADHANI
KARIBU msomaji wangu katika safu ya mahusiano, ili tuweze kubadilishana mawazo na kuelimishama
mambo mbalimbali yanayohusiana na masuala ya ndoa, uchumba, mafanikio na
changamoto zake.
KUCHELEWA
KURUDI NYUMBANI
Tabia ya mke
kutoka na kurudi nyumbani akiwa amechelewa mno au usiku tena wakati mwingine
bila kutoa taarifa kwa mumewe inakera wanaume wengi.
KUFANYA
MAPENZI NJE YA NDOA
Mume anapoona nyendo za mkewe hazieleweki anakuwa
mkali sana na na kusababisha mgogoro ndani ya nyumba na wakati mwingine husababisha mume kutofanya tendo la
ndoa na mkewe kwa kuhofia kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Mapenzi hupungua kwa
kiasi kikubwa na uaminifu kwa mkewe unakuwa haupo tena..
KUWA
NA MARAFIKI WABAYA
Katika ndoa mwanaume hapendi kuona mkewe ana
marafiki wanawake wenye mienendo mibaya, mfano malaya, wakorofi na wanaopeenda kutoka
‘out’ kila wiki kwa wa kuhofia kuambukizwa tabia mbaya, usaliti na kusahau
majukumu ya kulea familia na kumuhudumia mume.
KUPENDELEA WAZAZI WA UPANDE MMOJA
Mwanamke anayewajali zaidi wazazi wake pekee kuliko
wa mumewe, hata ndugu wanapaokuja upande wa mumewe hapendi ni tabia inayowakera wanaume wengi.
Tabia hii ikiendekezwa husababisha hata watoto
na husabisha mtafaruku katika
familia.
KUTOA
SIRI ZA NDANI NJE
Wapo baadhi ya
wanawake wanatoa mambo yao ya ndani
kwa mashoga zao bila kujali. Aidha kugawa vitu nje bila mpangilio na
kusahau majukumu ya nyumbani ni kero kwa mume.
MATUMIZI
MABAYA YA FEDHA
Baadhi ya
wanawake hutumia fedha za matumizi ya familia bila utaratibu na hawazingatii bajeti
na wa wakati mwingine hukataa fedha za matumizi
anazopewa kwa kisingizio kuwa hazitoshi hata pale anapoona hali ya
mumewe kwa wakati huo si nzuri kifedha lakini hapo upande wa pili unakuta
mwanamke huyohuyo anatumia gharama kubwa kujipamba na kufurahisha marafiki. Pia
tabia ya uongo na umbea huchukiza wanaume wengi kwa wake zao.
KUTOMJALI MUME
Baadhi
ya wake hujisahau katika kumjali mume, kwa mfano kunyooshea
nguo pasi, kumchagulia nguo ya kuzaa, kumuwekea maji ya kuoga na kula naye chakula pamoja na kutoshukuru
mume akimletea zawadi. Pia tabia ya kuwaachia kazi zote za ndani madada za kazi
hata zile apasazo mke kumfanyia mumewe hukera wanaume wengi na wakati mwingine
husababisha mume kuanza mahusiano ya kimapenzi na dada wa kazi.
KUFICHA
MAOVU YA WATOTO
Wapo baadhi ya kina mama wanaficha maovu ya watoto wao
hasa mabinti ili baba asimudhibu mtoto au kukemea. Hili linakera sana wanaume
kwani hawapendi tabia hizo na wakati mwingine hupunguza mapenzi kwa mkewe.
KUTOOMBA
MSAMAA
Baadhi
ya wanawake wanatabia ya kutoomba msamaha kwa waume
zao wanapokosea. Wengine huwa na tabia ya kufyonza, kutoitika wakiitwa, kukataa
kutembea au kukaa pamoja kujadili
masuala ya maendeleo na familia kwa ujumla na kutamani kuwa na maisha ya juu
kuliko uwezo wa mume.
USHAURI
Wanandoa wanapaswa kuwa makini katika maisha yao na uzingata misingi ya ndoa. Aidha, wanatakiwa
kuheshimiana, kuepuka kauli tata, kupendana, kusaidiana na kujadili kwa staha
tofauti ili kuwa ndoa yenye furaha na familia bora ya watoto wenye afya na
akili njema.
No comments:
Post a Comment