NA
ISSA RAMADHANI,
MCHEZAJI wa
timu ya Plaisance FC, Hussein Rashidi Bakari, anayekipiga katika timu
inayoshiriki ligi daraja la kwanza
nchini Seychelles,ametoa ushauri kwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars ,Salumu
Mayanja , kuwapa nafasi wachezaji wa wanaocheza soka nje ya Nchi ili kutoa changamoto kwa wachezaji wa ndani.
Miongoni mwa Timu alizowahi kuzitumikia hapa nchini
kabla ya kwenda nje ya nchi ni pamoja na klabu ya Makumbusho FC inayoshiriki
Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam na Simba Sc .
Mchezaji huyo
ambae ni zao la kituo cha kukuzia vipaji
kinachofahamika kwa jina la Makumbusho FC, ni mmoja wa vijana wanaoiwakilisha
vyema nchi hii na kupeperusha bendera ya
Taifa letu katika na kuifanya kusomeka vizuri kwenye ramani ya soka kama ilivyo kwa wachezaji
waliotangulia Samatta, Ulimwengu pamoja na Saimoni Msuva.
Haussein alianza maisha yake ya soka akiwa na umri
wa miaka kumi na nne {14} akikipiga kwenye kituo cha Soka cha Makumbusho,lakini
alifanikiwa kupata nafasi kwende kuichezea simba{B} badaae alipandishwa
kuichezea simba ya wakubwa lakini
akubahatika kupata nafasi katika kikosi cha kwanza .
Alikaa simba kwa kipindi cha miezi sita pamoja na
kukosa kucheza kwa kipindi hicho lakini alibahatika kupata nafasi ya kufanya
majalibio kwenye club ya Plaisance FC ya
nchini Seychelles timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini humo.
Katika majaribio, kijana huyo alifanikiwa kufaulu
majaribio hayo , wakati anaendelea kukipiga kwenye timu ya Plaisance FC aliitwa
kufanya majaribio kwenye timu ya
Foreshar FC ya ligi daraja la kwanza nchini Vietnam.
Katika kuonesha mapenzi yake kwa wachezaji, hapa
nchini alionekana kuvutiwa sana na Mlinzi wa Klabu ya Soka ya Simba, Mohamed
Hussein Zimbwe JR wakati ulaya akivutiwa sana na Mshambuliaji wa Kimataifa wa
Brazil na klabu ya PSG, Neymar JR.
Kwenye maisha hapakosi changamoto, mchezaji huyo
alisema moja ya changamoto ambazo zilikuwa kikwazo kwake katika maisha yake
ya Soka ni ugumu wa maisha ulikuwepo
kwenye Family yao ila haikumkatisha tama ya kwenda kufanya mazoezi akiwa
ajapata ridhiki hivyo hakusita kutoa shukrani kubwa na pongezi za dhati kwa
Kocha wake John Mashaka , Benchi la ufundi na timu nzima ya Makumbusho FC, kwa ushirikiano
mkubwa waliompa katika kukabiliana na changamoto alizozipitia .
Ushauri kwa Vijana wenzake wajitume kwa bidii
wakiamini soka linahitaji uvumilivu na mipango thabiti, hivyo aliishauri
Shirikisho la Soka la Tanzania (T.F.F) na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salumu
Mayanja, kuwapa nafasi wachezaji
wanaochezea nje ya nchi ili kutoa changamoto.
No comments:
Post a Comment