Kinondoni FC |
NA HASSAN RASHID.
KLABU ya Soka ya Kinondoni FC,
inayoshiriki daraja la pili yenye maskani yake Wilaya ya Kinondoni , Dar es
Salaam, imeiomba TFF kupitia upya na kuangalia kwa jicho la tatu katika kutatua
changamoto ya fidia za gharama kwa vituo
vya soka baada ya mchezaji kusajiliwa.
Kituo
hicho ambacho pia kinajishughulisha na kukuza soka la watoto (academia), ni
miongoni mwa vituo bora ambavyo vilifanikiwa kuzalisha nyota kadhaa wanaotumikia
ligi kuu Tanzania bara kwa sasa.
Kinondoni
Football Club, ilianzishwa mwaka 2010
baada ya kumalizika kwa mashindano ya Copa Coca Cola na kufanikiwa kupata jumla
ya Vijana 20 ambao waliunda timu hiyo.
Saleh Alawi |
“
Tunachangamoto kubwa sana hususani ya
wachezaji kuondoka bure japo sheria ipo , hili jambo kwa kweli liangaliwe upya,
tunatumia pesa nyingi kwa wachezaji lakini hata nusu hasara hatupati utakuta
mchezaji anajiunga timu kubwa kama Simba na Yanga huoni faida yake, na muomba
RaisKaria aliangalie kwa jicho la tatu”.Alisema Alawi
Aidha,
Alawi, alisema kuwa inauma sana mchezaji anasajiliwa Yanga au Simba moja kwa
moja anatambulishwa kama katokea Akademia hizo za Vijana jambo ambalo
linawakatisha tama ya kuendelea kukuza Vipaji.
“Kweli
Simba ua Yanga zinashindwa kulipa laki 5 kwa academia zinazozalisha wachezaji
ili watu waongeze bidii wazalishe wengine? Inauma sana inatukatisha tama hivyo
tuna muachia Mungu kwani tunapata usumbufu mkubwa kuliko gharama
tunazoziendesha”.Aliongeza Alawi
Miongoni
mwa wachezaji waliowahi kupitia kwenye kituo hicho cha KFC, ni pamoja na Ali abdallah a.k.a sonso Lipuli FC, Mbaraka Yusuph (Azam FC) Yahaya zaid (Azam
FC),Mohamedi Hussein Shabalala (Simba SC), Habibu Haji (Mbao FC), Daruweshi
Saliboko (Ashanti United) , Seif Adam (Coast Union) ,David Gama (JKT Mlale)
,Paulo Peter ( Azam FC) pamoja na Azizi Daud Nasri Aspire Aacademy ya Senegali
na wengine.
Alawi
alimpongeza Rais Karia kwa kuwa msikivu kitu ambacho alipenda kukiona
kinafanywa kazi chini ya Uongozi wake ni academia zote ziwepo na wataalamu
watakao leta maendeleo ya soka hapa nchini na kuwe na mkazo wa sheria ya
kuondoka kwa wachezaji kiholela.
No comments:
Post a Comment