NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Maliasili na Utalii hapa
nchini Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza
kusitishwa mara moja kwa oparesheni ya
kukamata mifugo katika pori Tengefu la Loliondo na kuagiza mifugo iliyokamatwa
kuachiwa mara moja.
Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla kushoto akizungumza. |
Aidha pia Kigwangala amesema hayo
leo na kusema mifugo mbalimbali ambayo imekamatwa na bado kufikisha mahakamani
iachiwe bila masharti yoyote na wafugaji waendelea kutumia vyanzo vya maji
ndani ya pori hilo.
Pia Waziri Kigwangalla anasema maamuzi hayo
aliyofanya ni hatua ambayo inalenga kutoa nafasi ya kushughulikia mgogoro huo
kwa njia ya mazungumzo.
Oktoba 19, 2017 Waziri Kigwangalla
alitoa agizo kuwa mifugo na matrekta ambayo yapo kwenye pori hilo Tengefu la
Loliondo viwe vimeondoshwa na kusema baada ya siku 7 mifugo na mali za watu hao
vingekutwa kwenye pori hilo basi Serikali ingevitaifisha.
No comments:
Post a Comment