Marekani.
NYOTA wa Muziki wa Hip Hop
nchini Marekani, Lil Wayne, amesema yupo mbioni kujitoa kwenye lebo ya studio
ya Young Money Rekodi kutokana na migogoro inayoendelea kwa sasa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya
habari kutoka Marekani , vilisema Wayne, alichukua uamuzi huo baada ya
kuwepo na migogoro baina yake na msanii mwenzake Bird man ambaye
yupo naye kwenye lebo hiyo ya Studio.
Wayne, alisema kama
migigoro hiyo haitapatiwa ufumbuzi basi lebeo hiyo ifungwe au itafutiwe shereia
ambayo itamaliza moja kwa moja matatizo yaliyopo ili kuleta amani kwenye lebo
hiyo.
lil Wayne |
. |
Sababu za ndani zilizomfanya Walyne kutaka kujitoa kwenye lebo hiyo ni pamoja na madai yanayoendelea dhidi ya Birdmani yakutaka kulipwa dola za kimarekani milioni nane.Katika hatua nyingine, Wayne, alionekana kutambulisha hati za umiliki wa Studio hiyo huku akiiomba mahakama kuteu mtu ambaye ataweza kusimamia shughuli za studio hiyo hadi pale kesi yao itakapomalizika au kuifungia studio hiyo.
Kesi hiyo inayoendela ni
kutokana na madai ya Lili Wayne kushtumu Studio hiyo kuwepo na upotevu wa
mamilioni ya pesa ambapo awali walingia kama ubia na msanii huyo kwani mwaka
2003 studio hiyo iliingia ubia na wasanii kama vile Drake pamoja na Nicki
Minaj.
.
|
Kumekuwa na mwenedelezo mbaya wa matumizi mabovu ya fedha katika studio hiyo ajambo ambalo lilizidi kukasirisha Lili Wayne na kupelekea kuaka kujitoa lakini upande wa Birdman alionekana kukaa kimya wakati mgogoro huo ukizidi kuendelea.
Drake, Nicki, Christina
Milian, na Lil Twist wote walisainishwa kwenye label ya Wayne. Mack
Maine pia ni msanii wa YME na rais wa label hiyo.
Pamoja na kwamba Birdman
ana umuhimu kwenye mafanikio ya Drake na Nicki, Weezy aliamini kuwa
mastaa hao wanapaswa kwenda naye kwasababu mikataba yao ni ya YME.
Kufanya issue hiyo kuwa
ngumu zaidi ni kuwa Cash Money ina mkataba wa usambazaji na wasanii wa Young
Money. Hiyo inamaanisha kuwa suala hilo itabidi limalizike mahakamani japo
vyanzo vimedai kuwa Lil Wayne hawezi kuondoka bila wasanii wake.
No comments:
Post a Comment