NA ISSA RAMADHANI.
KARIBU msomaji wangu katika safu hii yenye lengo la
kubadilishana na mawazo na kuelimishama mambo
mbalimbali yanayohusiana na masuala ya ndoa, uchumba na mafanikio na changamoto
zake.
Leo tutazungumzia mambo
muhimu ya kuzingatia kwa wale walio katika uchumba kabla ya kufanya uamuzi
mkubwa wa kufunga ndoa.
Kwa watu ambao wapo katika
kipindi cha mahusiano ya uchumba kwa muktadha wa kuwa mke na mume wanapaswa kuzingatia
yafuatayo kabla ya kuingia katika hatua hiyo.
Kwa pamoja fanyeni uamuzi
wa kupima afya zenu ili kujua hali zenu kabla ya kuingia katika ndoa pia
kuepuka kuambukizana magonjwa ya zinaa kama vile kaswende, Ukimwi ,gonorea na
endapo mmoja wenu au wote mkibainika kuwa na tatizo basi mnapaswa kutafuta tiba
kwanza kwa yale yanayotibika au ushauri nasaha yale yasiyotibika.
wanandoa pichani. |
Tendo hili la kupima
afya ni la muhimu sana kwa sababu ya kuwa chanzo cha madhara makubwa katika
familia ya wawili hao.
Madhara yanayoweza
kutokana na kuwa kwenye mahusiano ya kimwili kama mke na mume wakati mkiwa na
maradhi ni pamoja na gharama kubwa za matibabu, kuzaa watoto wenye matatizo, kusababisha umasikini katika familia kutokana na matumizi makubwa ya
rasilimali fedha katika kujitibu.
Fedha ambazo zitatumika
kujitibu baba, mama na watoto zingeweza kugharamia maendeleo ya familia kama
vile kuanzisha miradi ya kibiashara, kujenga nyumba, kusomesha watoto na
mengine muhimu.
Wachumba wanawajibika
kujali afya na kupata ushuri kwa wataalamu wa afya na wanasaikolojia mapema kabla ya kuingia katika ndoa ili matatizo yote yamalizwe kwa ushauri na tiba, hii itasaidia sana kuwa na
ndoa yenye furaha na afya.
Vijana wengi wa sasa hawazingatii haya na kujikuta wakiwa
katika majuto kwa kukurupuka kujikuta wanakutana na wakati mgumu hatimaye kuwa na migogoro katika ndoa.
No comments:
Post a Comment