NI jambo la kumshukuru Mungu kukutana tena katia safu hii. Leo tutazungumzia wanandoa waliopishana umri.
Kila uchao tumekuwa
tukishuhudia watu wengi wakifunga ndoa au kuchumbiana huku wakiwa na tofauti
kubwa ya umri iwe mkubwa au mdogo.
Wataalamu wanasema upo
umri wa kiafya unaotakiwa katika maamuzi ya kuishi kama wenzi ingawa ni muhimu
wapenzi au wanandoa kutokuwa na umri sawa kutokana na sababu za kibaiolojia,
kwamba umri wakati mwingine ni dawa muhimu ndani ya familia hasa kwa mwanamume
kuwa na umri mkubwa kuliko mwanamke.
Hata tafiti na tathimini
za kifamilia zinaonesha umuhimu wa umri mkubwa kwa mwanamume katika kuakisi
maandiko matakatifu ya quran na biblia, kwamba mwanamume ni kichwa cha nyumba.
Hapa suala nzima la uzoefu wa kiumri huzingatiwa katika umuhimu wake hasa
katika kusimamia, kuongoza na kushauri kaya au familia.
Hata
hivyo zipo baadhi ya changamoto ambazo zinaweza kufanyiwa kazi na mambo kuwa
sawa kwa wanandoa na wachumba wanaopishana umri:
Zinaweza kujitokeza tofauti za kimtazamo kwa
wanandoa kujikuta mmoja anapendelea kufanya hivi na mwingine hapendelei mambo
hayo.
Wanandoa wanaojivua kwenye maisha ya ndo yao. |
Kwa mfano, mwanamume mwenye umri mkubwa hupenda kujadili
masuala ya maendeleo, uwajibikaji wa kufanya mambo na kufuatilia zaidi masuala
ya familia, wakati kijana kutokana na msukumo wa umri wake mdogo anapenda zaidi kutoka ‘out’ na kuwa huru
kufanya mambo hata wakati mwingine yanayoweza kuhatarisha ndoa.
Mwanandoa kijana awe mume au mke anapendelea matumizi
ya mitandao, kustarehe, na kuchati hivyo kujikuta akivutana mara kwa mara
mwenzi wake.
Sehemu kubwa
ya hasa za Kiafrika zinaamini kwamba umri mkubwa wa mwanamke anapoolewa ni wa
msingi sana hasa linapokuja suala la kuzaa watoto. Watafiti wanasema
mwanamke mwenye umri mkubwa uwezo wake
wa kuzaa unapotea akiwa na miaka 40-50.
Kwa sasa baadhi ya wasichana wenye umri wa miaka
39-40 hupata mabadiliko ya mzunguko wa hedhi na wengine hukoma kuzaa kwasababu
ya ulaji wa vyakula vyenye kemikali ambazo hubadilisha mfumo wa mwili.
Ushauri wangu kwa wachumba waliopishana umri ni kutafuta
ushauri mzuri kwa wataalamu wa masuala ya ushauri, wanasaikolojia na watu
wengine wenye weledi mzuri wa mambo ya ndoa ili kuweka mambo sawa. Hii
itasaidia maisha yao ya ndoa kuwa mazuri, yenye maelewano na furaha.
Alamsiki.
No comments:
Post a Comment