Mbunge wa chama tawala
nchini Tanzania CCM Lazaro Nyalandu amejiuzulu wadhifa wake, na kusema kwamba
anataka kuhamia chama cha upinzani Chadema.
Aliyekuwa
Waziri wa Mali Asili na Utalii wakati wa serikali ya awamu ya Tano Bw Nyalandu, nchini Tanzania,Amesema kupitia taarifa kwamba amejuzulu nyadhifa zake zote ndani ya
chama cha mapinduzi CCM ikiwemo ubunge.
Lazaro Nyalandu pichani. |
Aidha pia Nyalandu ambaye kabla
ya maamuzi hayo ya kujiuzulu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini amesema
amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa na mwendo wa siasa nchini, ukiukwaji wa haki za kibinaadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu
dhidi ya raia na kutokuwepo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola Serikali,
Bunge na Mahakama.
Katika taarifa yake ya
kujiuzulu aliyoiweka katika ukurasa wake wa Facebook, Nyalandu amesisitiza
umuhimu wa nchi hiyo kupata katiba mpya.
"Naamini kwamba
bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili
ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa
mihimili ya Serikali," Amesema.
"Nimemua
kujiuzulu Kiti cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa
uchaguzi mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona
inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania.
"Ni imani yangu,
kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya
Watanzania leo."
Nyalandu anaingia
katika orodha ya mkururu wa viongozi wa juu wa CCM waliokihama chama hicho na
kuhamia chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema tangu mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment