NA ISSA RAMADHANI.
MUOGELEAJI shujaa
kutoka Tanzania, Collins Saliboko,
ambaye hivi karibuni alitwaa jumla ya medali kumi na sita katika mashindano ya
kuogelea kwenye cana kanda ya tatu Afrika
Collins Saliboko pichani. |
Mashindano hayo yalifanyika Tanzania kwenye bwawa la kuogelea la Hopac Jijini Dar es salaam ambapo jumla ya timu nane zilijitokeza kushiriki.Nchi zilizoshirik mashindano hayo ni nchi za Afrika ya Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan ya Kusini, Djibout, na mwenyeji na bingwa mtetezi nchi ya Tanzania.
.
Akizungumza hivi
karibuni mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo hapa nchini, Saliboko, alisema kuwa mashindano
hayo yalikuwa magumu sana licha ya kujaribu kuibuka na medali kadhaa lakini kwa
sasa atahakikisha anaibuka kinara wa medali za dhahabu kwenye ya mashindano ya
Jumuiya ya Mdola yatakayofanyika Huko Australia mwakani, Olimpiki ya Vijana ya
Mwezi Oktoba na kufanyika Nchini Argentina.
Collins,
alifanikiwa kutwaa jumla ya medali 16, ambapo kati ya medali 13 zikiwa ni za
shaba kwa nafasi ya pili wakati medali tatu zikiwa za dhahabu.
Katika mashindano
hayo yaliyomalizika hivi karibuni, Saliboko alifanikiwa kutwaa medali nyingi
mara baada ya kuwa katika mashindano kumi na sita aliyoshiriki kitu
kilichomfanya afikishe wingi wa tuzo hizo tofauti na wenzake.
Baadhi ya
waogeleaji wengine waliojinyakulia medali hizo za dhahabu ni pamoja na Elia Imhoff Natalie, Emma Imhoff,
Tara Behnsen, Marin De Villard na kwenye ‘relay’ walikuwemo Sonia Tumitto,
Collins Saliboko, Hilal pamoja na Emma
Imhoff.
“Mashindano ni
magumu sana, ushindani ulikuwa mkubwa sana pamoja na kuwa na uhakika wa 100% ya
kushinda, waogeleaji wetu walifanya vyema katika mashindano ya awali na
tuliongoza kwa kutwaa medali licha ya kuwa nje ya mipango yetu”.Alisema
Saliboko
Miongoni mwa shule
alizowahi kupitia katika kuhakikisha anafanya vyema kwenye mchezo wa kuogelea
ni pamoja na Mikocheni East Africa School, Shinyanga Shule ya Savana, pamoja na
Shule ya Morogoro ambapo kote alikutana na mafunzo bora yaliyomfanya kutwaa medali
hizo.
Ndoto yake kwa sasa
ni kuhakikisha anajipanga vyema kunyakuwa medali za dhahabu na kuiletea heshima Tanzania kwenye michuano ya
Olilimpiki pamoja na Jumuiya ya Madola mwaka.
No comments:
Post a Comment