NA MOHAMEDI
NG`OULA .
CHAMA cha Siasa cha ACT Wazalendo kimemshauri Waziri wa Viwanda
na Biashara, Charles Mwijage kusimamia
bei ya zao la mbaazi kutokana na umuhimu wa zao hilo katika kukuza kipato cha
mwananchi na taifa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage(kulia) akipata maelezo kwa mwendesha mitambo wa kampuni ya TBL, Mecky Mlay alipotembelea. |
Ushauri huo jijini Dar es salaam na
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho Ado Shaibu, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya
habari juu ya utafiti ulifanywa na chama hicho kuhusu hali
ya soko la mbaazi hapa nchini.
Akifafannua, alidai kuwa serikali
inasuasua kutumia mkataba kati yake na
India wa kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuuza mbaazi nchini humo kitendo
ambacho kinasababisha wakulima kukosa uhakika wa kilimo kutokana na kusuasua
kwa bei.
Wakulima wa kilimo cha pamba pichani. |
Kwa mujibu wa katibu huyo, uzalishaji
mkubwa wa mbaazi nchini umechochewa na India kabla na wakati wa ujio wa Waziri Mkuu
wa nchi hiyo, Narendra Modi hapa nchini ambapo wakulima na
wafanyabiashara walihakikishiwa soko, ingawa
suala hilo halikutiliwa mkazo na mbaazi nyingi za wakulima kuozea
shambani.
“Tulielezwa kwamba Tanzania haistahili kuzuiwa
mbaazi zake kwa sababu zuio husika haligusi nchi zenye mahusiano mahususi
na kuuza mazao India. Sisi tuna makubaliano ya kupeleka mazao India wa mwaka
2000… ni jambo la kushangaza kuwa serikali imeshindwa kulifuatilia tangu lilipo
jitokeza mwezi wa nane mwaka huu,”alisema Shaibu.
Katibu huyo, alisema alisisitiza
umuhimu wa serikali kutafuta masoko
mapya ya zao la mbaazi kwenye nchi
tofauti na India kama vile Afrika Kuusini, Canada, Uingereza na Marekani
na kutumia mkataba wa India ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuuzia
mbaazi nchini humo.
“Serikali ifanye mazungumzo na
serikali ya India ili kuwanusuru
wakulima, tunatambua Tanzania na India ni marafiki tangu uhuru wa Taifa letu,
ni vyema tuyatumie mahusiano haya
kuhakikisaha tunalinda soko la wakulima wetu sambamba na kutafuta masoko
kwinginepo kwa kutumia mkataba huu ili kuziaminisha nchi hizo uhakika wetu wa
uzalishaji, ”.alisisitiza.
Katika hatua nyingine,
Katibu huyo wa ACT alishauri kufunguliwa kwa viwanda vya usindikaji wa bidhaa
zinazotokana na mbazi kama biskuti na keki badala ya kufikiria kuuza nje pekee
jamboa ambalo haliakisi kuongeza ajira na
sera ya Taifa la Viwanda.
Hivi karibuni zao la mbaazi limekuwa
likilalamikiwa kushuka kutoka Shilingi 2, 500 kwa kilo msimu
wa mwaka 2016 hadi shilingi 2,000 kwa kilo kwa mwaka huu kwenye mikoa mbalimbali
nchini jambo ambalo limewaathiri wa wakulima wengi kutokana na kulima mbaazi
kwa wingi huku soko likisuasua na kusababisaha hasara kubwa.
No comments:
Post a Comment