Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Ndugu Humphrey Polepole amerusha
jiwe gizani kwa Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe kwamba anajua wakati huu
anapitia wakati mgumu sana ndani ya chama ndiyo maana anatapatapa katika suala
la makubaliano kati ya serikali na Kampuni ya Uchimbaji madini ya Barrick.
Akifanya mazungumzo ndani ya Ofisi yake na
EATV, Polepole Alisema kwamba kitendo
cha Mbunge huyo kwenda kuzungumza kwenye chombo cha habari na kuuhadaa umma
kwamba madini yataendelea kuwa madini ya watu wa nje, yeye
hana tatizo naye kwani anafahamu wazi kwamba chama kinaenda kumfia hivyo
watu wamuelewe.."Naomba mumuelewe huyu bwana, anapitia wakati mgumu. Chama kinamfia tumuelewe sana. Watu wote wenye uelewa mpana walioshiriki katika kukianziasha chama wote wameondoka na wameondoka kwa masikitiko ya kwamba chama kimepoteza dira. Asubiri kuona matokeo ya maendeleo yanayoletwa na serikali. Mfama maji haishi kutapatapa ni sehemu ya asili ya ubinadamu. Namwambia asubiri kuona maendeleo yatakuja kutokana na makubaliano haya makubwa" Polepole.
Aidha Polepole amesema kwamba Zitto ameshiriki katika kutunga sheria tatu ndani ya Bunge kuhusu madini kisha akaenda ulaya kusema kwamba madini yatazidi kuchukuliwa na wageni ni kuuhadaa umma kwani katika sheria waliyoitunga ilikuwa ni ya kutamka kwamba madini yaliyopo ardhini ni mali ya watu wa Tanzania.
Ameongeza pia Sheria ya pili Mh. Kabwe aliyoshiriki ni pamoja na ile ya Kuipa Mamlaka Bunge kutazama masuala ya madini vizuri na sheria ya tatu ikiwa ni kuboresha sheria za kodi ikiwa mapato na bima lakini kwa sababu chama kinaenda kumfia hivyo hataweza kuacha kudandia hoja hata kama hazina mashiko.
No comments:
Post a Comment