"Serikali yawabana wamiliki wa nyumba." - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, 5 December 2017

"Serikali yawabana wamiliki wa nyumba."



 Image result for lukuvi
NA ISSA RAMADHANI,
SERIKALI  imesema kuwa ni marufu kwa wamiliki wote wa nyumba nchini kuwalipisha wapangaji wao kodi ya mwaka mzima badala yake iwape fursa ya kulipa kodi hiyo kwa mwezi mmoja mmoja.
Related image
Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ufunguzi wa jengo la ofisi za makao makuu ya shirika La nyumba nchini (NHC).

Amesema kuwa ni wakati Sasa kwa wamiliki wa nyumba nchini kuwapa uhuru wapangaji wao kulipa kodi kwa mwezi mmoja mmoja ili kuweza kuwapatia unafuu.

“Ni wakati sasa wa kuwapa uhuru wapangaji kulipa kodi ya mwezi mmoja mmoja badala ya miezi sita au kumi na mbili kama ilivyokuwa mwanzo,”amesema Lukuvi

Hata hivyo, Lukuvi ametumia nafasi hiyo kuwaonya madalali wote kulipa kodi kwani wamekuwa wakifanya kazi na kuchukua 10% ya pato lakini hawalipi Kodi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot