Shashi Kapoor ameigiza filamu zaidi ya 50.
INDIA,Mumbai
MWIGIZAJI
mkongwe wa Bollywood Shashi Kapoor
amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.Kapoor, aliyeigiza katika filamu
maarufu kutoka India kama vile Deewar na Kabhie Kabhie, amekuwa akiuguza kwa
muda na alikuwa amelazwa hospitali.
Shashi anatoka familia ya Kapoor ambayo imetawala tasnia ya filamu za Kihindi kwa miongo mingi. Alishinda tuzo nyingi za filamu za taifa na alitunukiwa tuzo kuu ya heshima inayopewa raia na serikali ya India mwaka 2011, tuzo ya Padma Bhushan.
Ambapo Aliigiza pia katika filamu kadha za Uingereza na Marekani.Kapoor amefariki akitibiwa katika hospitali ya Kokilaben Dhirubhai Ambani mjini Mumbai.Takwimu zinaonyesha amecheza filamu zaidi ya 50.enzi za uhai wake.
Hata hivyo mpwa wake Randhir Kapoor ameambia Press Trust of India kwamba Kapoor amekuwa akitatizwa na figo kwa miaka mingi.
Alikuwa amemuoa mwigizaji mwingereza Jennifer Kendal, ambaye kwa pamoja walianzisha ukumbi maarufu wa sanaa Mumbai wa Prithvi mwaka 1978
No comments:
Post a Comment