Kikosi cha Singida united |
NA ISSA RAMADHANI,
KLABU ya Singida United, leo wametangaza orodha ya wachezaji waliowaacha katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili,msimu huu, ambacho kilifunguliwa Novemba 15 na kitafungwa Desemba 15 mwaka huu.Ambapo Miongoni mwa wachezaji hao waliotemwa ni mshambuliaji Atupele Green ambaye aliwahi kuzitumikia Kagera Sugar na JKT Ruvu zote zinashiriki ligi kuu soka Tanznaia bara.
Mchezaji mwingine alietemwa na klabu hiyo ya mjini Singida ni Pastory Athans ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Simba, huku Mohammed Titi na Frank Zacharia wakitolewa kwa mkopo.ili kuimalisha viwango vyao.kuleta ushindani katika ligi kuu Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment