MSANII wa Muziki Bongo hapa
nchi , Nandy amesema anaweza ku-date na
Bill Nass ila siyo Dogo Janja kutokana na urafiki wao kuwa wa karibu zaidi.
Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa ‘Kivuruge’ ameiambia The Playlist, Times FM kuwa Bill Nass huwa anamvutia zaidi ya Dogo Janja, hivyo anaweza kumtazama kwa jicho la pili.
“Dogo Janja ni rafiki yangu, Dogo Janja hayupo kabis labda Bill Nass watu
wanavyomzungumzia naweza nikakaa mwenye pembeni nikasema ok, labda nikamtazama
kwa jicho la pili lakini Dogo Janja siwezi hata nikapoteza muda kumfikiria kwa
sababu ni nigger wangu” amesema Nandy.“Si kwa kwamba (Dogo Janja) siyo type yangu, ni kijana mwenzangu lakini ni rafiki yangu ambaye najua matatizo yake na yeye anajua ya kwangu tuna-share kiasi kwamba siwezi hata kumfikiria lakini Bill naweza kumfikiria” amesisitiza.
Katika hatua ngingine Nandy ameeleza licha ya kuwepo tetesi nyingi kuwa
ana-date na Bill Nass hakuna jambo kama hilo na Bill Nass hajawahi hata
kumueleza kuwa anamuhitaji.
No comments:
Post a Comment