Msajili wa Vyama vya Siasa apelekwa Mahakamani na Chama cha ‘Mtikila’ - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, 22 November 2017

Msajili wa Vyama vya Siasa apelekwa Mahakamani na Chama cha ‘Mtikila’


Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi.  

NA YUSUPH MWAMBA,

CHAMA CHA DEMOCRATIC (DP), kimeomba kibali cha kumfungulia mashtaka msajili wa Vyama vya Siasa nchini. jijini Dar es salaam, Tanzania.

Chama hicho ambacho kiliasisiwa na Mchungaji Christopher Mtikila ambaye sasa ni marehemu kimewasilisha maombi Mahakama Kuu, kikiomba kibali cha kumfungulia kesi msajili wa Vyama vya Siasa kikimtuhumu pamoja na mambo mengine kuingilia mambo yake ya ndani.

Maombi hayo yaliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dar es Salaam dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) yamepangwa kusikilizwa na Jaji Kiongozi, Ferdinand Wambali, Jumatatu ijayo.

Kwa mujibu wa hati ya maombi ya faragha yaliyowasilishwa mahakamani hapo chama hicho kimefikia uamuzi huo baada ya msajili kukiandikia barua mbalimbali ikiwemo ya kubatilisha mkutano mkuu wa chama uliofanyika Mei 26.

Pia, chama hicho kinapinga hatua ya msajili kutowatambua viongozi wa chama hicho waliochaguliwa katika mkutano huo na badala yake kuwatambua wasio viongozi na wasio wanachama.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot