Tambua madhara ya kutumia Simu ya Smartphone kwenye Giza - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, 22 November 2017

Tambua madhara ya kutumia Simu ya Smartphone kwenye Giza

NA ISSA  RAMADHANI,


WATU  wengi  hapa duniani tuanpenda kutumia simu mahali ambapo pana giza mfano room pa kulala au sebulenina maeneo mengine kwa muda mrefu, sisi vijna tunapenda “kukuchati”.  Kuchati huku nyakati za giza wakati taa imezimwa huwa na madhara yafuatayo.

Kwa sasa, idadi ya wagonjwa kuanzia miaka 30-40 wanatafuta matibabu makubwa. kutokana na matumizi ya simu za mkononi (smart phone) gizani. hasa vijana.

MTAFITI Profesa Li Li, kiongozi wa hospitali ya macho huko singapore amesema: anasema mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dk 30 na kuendelea inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli macho na hivyo kusababisha saratani na kushindwa kuona kabisa.

Kwa sababu wakati wa kutumia simu mahali penye giza huwa tunayalazimisha macho yetu yaweze kuona ya uwezo wake. Na ndiyo maaana kuna wakati unaweza ukatumia simu muda mrefu mahali penye giza mara baada ya kuacha kutumia simu utaona kama giza limezidi zaidi. Hali hiyo huyafanya macho yako yaanze kurudi katika hali ya ukawaida.

Pia utumiaji wa simu kwenye giza husababisha Kupata saratani ya macho. Hivyo ili uweze kuepuka saratani hivyo ni bora tuache kutumia simu za mikononi gizani ili tujikinge. Simu za mikononi (smartphone) zenye mwanga mweupe sana karibu na macho gizani, unabadili mfumo wa seli macho na kupelekea matatizo ya saratani ya macho.

Proffessor Li Li amesema dalili za mbadiliko wa seli macho mara nyingi wanazigundua watu wenye umri mkubwa (wazee), ila kwa hivi sasa zinagunduliwa hata na kwa vijana wadogo. Hasa kwa wenye umri wa kuanzia miaka 30-40 wanaongezeka kwa asilimia 3% na wote hawa ni watumiaji wa simu za mikononi (smartphone) kupitiliza.

 Utumiaji wa simu inaweza sababisha na ugonjwa wa macho makavu, mtoto wa jicho na mwisho kupelekea kupoteza kuona.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot