MADRID, HISPAIN
MCHEZAJI wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo amekataa kuzungumza na vyombo vya habari baada ya kufanikiwa kufunga
mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 6-0 ilioupata timu yake dhidi ya APOEL
kwenye Ligi ya Mabingwa
Ronaldo alipofuatwa na wanahabari baada ya mchezo
huo alikataa kuongea hadi pale walipomganda zaidi lakini alisisitiza kuwa
hawezi kuongea chochote na hana raha ya kufanya mahojiano na wanahabari.
“Sihitaji kuongea, sihitaji kuhojiwa juu ya lolote, nimechoshwa na nafadhaishwa
na namna ambavyo mnabadilisha maneno, leo naweza kuongea jambo moja kisha
mkaandika tofauti kabisa na nilichosema”, amesema Ronaldo mbele ya wanahabari
waliokuwa wakimzonga kwenye uwanja wa GSP.
![]() |
| Ronaldo akimtoka mchezaji wa APOEL katika mchezo wa jana uefa champ , Real madrid waliifunga goli 6-0 |
Hatua ya Ronaldo kugoma kuongea na wanahabari ni matokeo ya habari zilizoripotiwa hivi karibuni kuwa Ronaldo ana ugomvi na nahodha wake Sergio Ramos baada ya Ronaldo kukaririwa akisema “Real Madrid haifanyi vizuri kwenye La Liga kwa sababu ina wachezaji wengi ambao si wazoefu baada ya kuwauza Alvaro Morata na James Rodriquez” kitu ambacho Ramos alikipinga kwa nguvu.
Baada ya kufunga mabao mawili kwenye
ushindi wa mabao 6-0 sasa Ronaldo ameifungia Real Madrid mabao 98 kwenye mechi
96, akimzidi mshindani wake Lionel Messi ambaye ameifungia Barcelona mabao 97
kwenye mechi 119.


No comments:
Post a Comment