NA ODRIAN NICHOLAUS
KUMEKUWA na dhana katika jamii kuwa dagaa ni kitoweo au mboga ya watu
masikini. Bahati mbaya sana ni kwamba wengi wao hawana uwelewa tiba ya mboga
hiyo, yumkini ndio sababu ya kuwapo kwa dhana hiyo.
Dagaa ni kitoweo kinachopatikana kwa
urahisi kwa jamii nyingi hapa nchini kutokana na uwingi wa kitoweo hicho
sokoni, vibanda vya biashara ndogondogo maarufu kama magenge na sasa kutokana
na kukua kwa biashara pia huuzwa kwenye maduka makubwa ya biashara (super
markets).
Watalaamu wa afya na lishe wanasema
dagaa ni chakula muhimu katika mwili wa binadamu bila kujali kipato kutokana na
faida zake mwilini, ambazo wanabainisha kuwa ni pamoja na kuzuia shambulio la
moyo.
Hiyo ni kwasababu ya kuwapo kwa
virutubisho vingi kwenye dagaa kama vile kiwango kikubwa cha
kirutubisho aina ya Omega-3 (Fatty Acid) kilichomo .
Mmoja wa watafiti hao, Dk.
Edward Group wa nchini Marekani anaandika makala ya matokeo ya utafiti kuhusu
kitoweo hicho kuwa kutokana pia na kiasi kingi cha madini ya kalishiam
yaliyomo kwenye dagaa husaidia kuimarisha mifupa mwilini.
Dk. Group ambaye pia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Global Healing cha nchini humo anasema katika
makala yake hiyo kuwa dagaa wana vitamin D ambayo huwa nadra sana kupatikana
kwenye lishe ya kawaida.
Vitamin D pia huimarisha afya ya
mifupa ikisaidiana na madini ya fosforas yaliyomo kwenye dagaa, alisema.
Zaidi, dagaa ni chanzo kizuri
cha Vitamin B12 baada ya maini ambayo ndio chanzo kikuu cha vitamin hivyo.
Vitamini B12 hufanya kazi kubwa ya
kuboresha ustawi wa moyo na hivyo kuwa chakula kizuri cha kumpa ahueni mgonjwa
husika au kinga madhubuti mlaji dhidi ya magonjwa ya moyo.
Watafiti wengine nchini humo pia walibaini kuwa miongoni mwa vidhibiti vya magonjwa ya saratani ni pamoja na dagaa kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya kalisiam ambayo husaidia kupambana na seli zinazosambaza saratani mwilini.
Wanasema dagaa zina kiasi kingi cha protini, hudhibiti upungufu wa protini mwilini, ilisema sehemu ya makala.
Watafiti wengine nchini humo pia walibaini kuwa miongoni mwa vidhibiti vya magonjwa ya saratani ni pamoja na dagaa kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya kalisiam ambayo husaidia kupambana na seli zinazosambaza saratani mwilini.
Wanasema dagaa zina kiasi kingi cha protini, hudhibiti upungufu wa protini mwilini, ilisema sehemu ya makala.
Protini husaidia uzalishaji wa
‘amino acids’ ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa chembe hai mwilini na
uimarishaji wa mfumo wa kinga ya mwili (body immune system) na kujenga mwili.
“Licha ya kuwa dagaa wana faida
katika mwili wakati wa ulaji lakini pia ni watamu mdomoni na huleta hamu ya
kula na kukufanya ule chakula kingi na kushiba,”anasema Dk. Group.
Katika tafiti nyingi za magonjwa ya
moyo na tiba zake, virutubisho vya Omega 3 vimeonekana kuwa dawa au kinga
muhimu ya magonjwa ya moyo ambayo yamekuwa yakitumia mamilioni ya pesa katika
tiba. Tumekuwa tukishuhudia wagonjwa wengi hapa nchini wakisafirishwa nje ya
nchi hasa huko Apollo nchini India kwa matibabu. Inaelezwa kuwa chanzo
kikuu cha virutubisho hivyo ni viumbe wa majini ikiwamo samaki na dagaa.

No comments:
Post a Comment