![]() |
| Waziri wa mambo ya ndani ya nchi ,Dokta Mwigulu Nchemba pichani |
NA MWANDISHI WETU.
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania, Dkt Mwigulu Nchemba amewakosoa upinzani
kutumia tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu
Lissu kama ajenda katika kampeni za uchaguzi wa marudio na kusema kwamba chama
hicho kimefilisika.
Akiwa Masasi katika kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa tiketi ya CCM, Dkt
Nchemba amesema kwamba kitendo hicho cha Chadema kufanya kila mahali tukio la
Lissu kama ndiyo ajenda atakwenda kuwaambia wakazi wa Singida wawaangalie
vizuri watu hao.
"Mimi nitaenda kuwaambia wana
Singida kwamba tuwaangalie vizuri hawa watu. Wao ni mwenzao kwenye Chama
sisi ni ndugu yetu na tunatoka sehemu moja. Inawezekanaje wawe wanafurahia
tukio hilo? Kama kuna kitu walikuwa wanataka kitokee ili warushe maneno kwa
serikali" amesema Dkt Nchemba.
Aidha akiendelea Nchemba amesema Chadema wanamuona kama Lissu mtaji ndiyo maana
hata polisi walipomtaka dereva wake ili kuweza kumhoji wameamua kukaa naye
huko.
Pamoja na hayo Nchemba amewata watu wakapige kura bila kuhofia fujo zinazoweza
kufanywa na wanachadema kwani serikali ipo kwa ajili ya kusimamia sheria.
"Wamezoea kufanya fujo.
Nendeni mkapige kura akitokea mtu atakayethubutu kukughasi wewe mkariri sura
alafu sisi tutamfundisha ustaarabu wa vyama vingi. Anayefanya fujo atakutana na
mkono wa sheria. Na uzuri vijana wangu wapo hapa atakayethubutu kufanya fujo,
Muwaonyeshe kwamba mmepitia mafunzo" Nchemba
Hata hivyo Nchemba amewataka wananchi hao kuichagua CCM kwa kazi nzuri
inayofanya na kuwaamba kuuchagua upinzani wakitegemea itashinda ni sawa na
kujeruhi nafsi.

No comments:
Post a Comment