Kinondoni FC yalilia sheria kandamizi ya wachezaji - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday 13 December 2017

Kinondoni FC yalilia sheria kandamizi ya wachezaji

                                                                                Kinondoni FC


NA HASSAN RASHID.
KLABU ya Soka ya Kinondoni FC, inayoshiriki daraja la pili yenye maskani yake Wilaya ya Kinondoni , Dar es Salaam, imeiomba TFF kupitia upya na kuangalia kwa jicho la tatu katika kutatua changamoto ya  fidia za gharama kwa vituo vya soka baada ya mchezaji kusajiliwa.

Kituo hicho ambacho pia kinajishughulisha na kukuza soka la watoto (academia), ni miongoni mwa vituo bora ambavyo vilifanikiwa kuzalisha nyota kadhaa wanaotumikia ligi kuu Tanzania bara kwa sasa.

Kinondoni Football Club, ilianzishwa  mwaka 2010 baada ya kumalizika kwa mashindano ya Copa Coca Cola na kufanikiwa kupata jumla ya Vijana 20 ambao waliunda timu hiyo.
                                                                       Saleh Alawi
Akizungumza na Gazeti la Raia Tanzania, Mwalimu na Mmiliki wa kituo hicho cha KFC, Saleh Alawi, alisema kama soka la Tanzania linahitaji maendeleo lazima watoe kipengele cha mchezaji kuondoka  huru kwenye vituo hivyo kwani wanajikuta wakiwalea watoto kwa gharama kubwa faida hakuna.
“ Tunachangamoto  kubwa sana hususani ya wachezaji kuondoka bure japo sheria ipo  , hili jambo kwa kweli liangaliwe upya, tunatumia pesa nyingi kwa wachezaji lakini hata nusu hasara hatupati utakuta mchezaji anajiunga timu kubwa kama Simba na Yanga huoni faida yake, na muomba RaisKaria aliangalie kwa jicho la tatu”.Alisema Alawi

Aidha, Alawi, alisema kuwa inauma sana mchezaji anasajiliwa Yanga au Simba moja kwa moja anatambulishwa kama katokea Akademia hizo za Vijana jambo ambalo linawakatisha tama ya kuendelea kukuza Vipaji.
“Kweli Simba ua Yanga zinashindwa kulipa laki 5 kwa academia zinazozalisha wachezaji ili watu waongeze bidii wazalishe wengine? Inauma sana inatukatisha tama hivyo tuna muachia Mungu kwani tunapata usumbufu mkubwa kuliko gharama tunazoziendesha”.Aliongeza Alawi
mazoezi ni baadhi ya wachezaji ,Kinondonin Fc 

Miongoni mwa wachezaji waliowahi kupitia kwenye kituo hicho cha KFC, ni pamoja na  Ali abdallah a.k.a sonso Lipuli FC,  Mbaraka Yusuph (Azam FC) Yahaya zaid (Azam FC),Mohamedi Hussein Shabalala (Simba SC), Habibu Haji (Mbao FC), Daruweshi Saliboko (Ashanti United) , Seif Adam (Coast Union) ,David Gama (JKT Mlale) ,Paulo Peter ( Azam FC) pamoja na Azizi Daud Nasri Aspire Aacademy ya Senegali na wengine.

Alawi alimpongeza Rais Karia kwa kuwa msikivu kitu ambacho alipenda kukiona kinafanywa kazi chini ya Uongozi wake ni academia zote ziwepo na wataalamu watakao leta maendeleo ya soka hapa nchini na kuwe na mkazo wa sheria ya kuondoka kwa wachezaji kiholela.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot