KWA mara nyingine nakukuribisha
msomaji katika safu hii ya mahusiano ili
tuweze kubadilishana mawazo na kuelimishama kuhusu masuala mbalimbali
yanayohusiana na ndoa na uchumba, mafanikio na changamoto zake.
Leo
tutazungumzia mambo ya kufanya ili kuboresha ndoa au mahusiano kwa kuyajua mambo yanay
sababisha mahusiano ya kimapenzi kuvunjika.
NA ISSA RAMADHANI
Tabia
hizi ndizo zinasababisha mahusiano ya watu wengi kuvunjika, hata ndoa kuharibika
baada ya kukosekana uvumilivu. Hali hiyo husababisha maumivu, vidonda vya
mapenzi na hata vifo na kuwafanya watu wengine kuchukia kupenda au kupendwa
katika maisha yao.
Mawasiliano duni
Kutokuwa
na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako, husababisha matatizo kujitokeza pia ukishindwa kukaa na kujadili mfano
kumpigia simu, kuonana, kutoka “out” na kuzungumza ili kupata ufumbuzi ndio
mwanzo wa kuachana na mwenzi wako, huwa si lazima akuambie utaona mazingira
yanabadilika na mwisho mnaachana.
Maelewano
Hili ni
jambo jema ni muhimu kwa afya ya ndoa au uchumba wenu. Kuwa tayari muda wote
kumsikiliza mwenzako anachozungumza.Baada ya ratiba ngumu za siku kuwa na hamu
ya kumsikiliza mwenzako na kumuuliza maswali mbalimbali.kumbuka wakati
mwinginemke au mume wako anahitaji kukuuliza au kukusikiliza, epuka sana kutoa
hitimisho wewe tu!, fungua masikio yako na msikilize kile anachosema mwenzako.
Kujali
Hapa
kuna shida sana, wapo baadhi ya wapenzi wamo kwenye mahusiano lakini hawajali
maumivu ya mwenzie. Mfano anumwa, anamatatizo au huzuni hiki ndio kipindi cha
kukaa na kumliwaza, lakini asilimia kubwa sana wako “busy” na mambo yao.
Ubishi
Tabia
hii hivi sasa inashika kasi sana kwenye mahusiano mengi. Hata katika jambo
ambalo kueleweshana lazima kuwe na ubishi usiokuwa na tija. Kwa mke na mume
kushindwa kuelewana huharibu uhusiano. Kila mmoja ajaribu kujishusha ili kupata
muafaka katika jambo mlilotofautiana.
Kutokubali makosa
Hakika
utakubaliana na mimi kuwa baadhi ya wapenzi wana tatizo hili la kutokubali kosa
na kujisahihisha japo kuna ushaidi. Kukubali makosa, kuomba msamaha na
kujisahihisha na jambo zuri katika kuimarisha mahusiano.
Kutoonesha upendo
Onyesha
unampenda sana mke au mume wako daima. Kila siku hakikisha unadhihirisha upendo
wako kwake usichoke. Mbusu mke au mume wako, mkumbatie kila mara kama ishara ya
upendo. Kama mtapendana kwa dhati basi bila shaka mtaheshimiana na kila mmoja
atamthamini mwenzake. kila siku tafakari kwa nini ulimpenda yeye tu na wala si
mwingine, hii itakufanya umpende zaidi mke au mume wako.
Kutikuwa muwazi
Kukaa
na kuelezana mambo unayopenda na usiyoyapenda kwa mwenzi wako kwenye mahusiano
ni jambo zuri kwani husababisha kujua nini
ukimfanyia mwenzio anakuwa na furaha na nini kina mkera. Kuwa muwazi
katika mipangoya kustawisha mahusiano
yenu na maendeleo kwa kushirikishana.
Kustahiana
Kitendo
cha kumgombeza mwenzi wako mbele za watu kinaonyesha picha mbaya
mnavyoishi kwa jamii
inayowazunguluka.Wapo badhi ya wapenzi bila kupishana kauli hajisikii raha. Kila mtu hapendi malumbano,
ugomvi na kudhalilishwa.
Mthamini mwenzako
Kila mmoja anapaswa kutambua thamani
ya mwenzi wake katika maisha. Mnapaswa kuelewana na kujuana tabia zenu ili kujenga maisha bora
ya mapenzi yenu. Mzungumze kwa lugha upole na upendo.
Shugulikia matatizo yako yanayokusumbua kwani
hapa dunia kila binadamu aliyekamilika
anitaji kuwa na mke, mume na hatimaye familia. Badilika sasa.
No comments:
Post a Comment