Shilole awataka wasanii wapambane na hali zao - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday 8 February 2018

Shilole awataka wasanii wapambane na hali zao

NA ISSA RAMADHANI

MSANII wa miondoko ya pwani hapa nchini Zena Yusuf Mohammed  maarufu “ Shilole” , amesema wasanii wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kukabiliana na hali ya kiuchumi iliyopo.

Shilole,  ambaye hivi karibuni alifunga ndoa na muwewe Uchebe, aliwataka wasanii wakaze buti na kuangalia fursa zilizopo ili kukabiliana na hali ya uchumi, kwani sanaa ya sasa ni ngumu ukilinganisha na  miaka iliyopita.



Akizungumza na mwandishi, Shilole , alisema mwaka jana soko la sanaa lilikuwa zuri ukilinganisha uchumi ulikuwa unaoneka tofauti sasa ambako kila msanii anatakiwa ajitume na kupambana na hali yake katika kujitengenenezea maisha yake na familia yake.

“Muziki wa sasa sio wa kubweteka, lazima ujitume, utengeneze nyimbo nzuri zitakazo wavutia mashabiki kama msanii atatoa ngoma mbaya basi hali ya kiuchumi itaendelea kuyumba kila siku”,alisema Shilole

Alisema kuwa, wasanii walikuwa wakitegemea sana shoo za  nje na za ndani, ila kwa sasa hali ni tofauti wananchi hawana fedha za kuingia kwenye kumbi za starehe, watu wengi wanafikiria jinsi ya kuhudumia familia zao kuliko starehe, hivyo kama wanataka pesa ni lazima wafanye kazi nzuri zitakazowavutia mashabiki.

Aidha, Shilole, yupo mbioni kuachia nyimbo ambayo hakumshirikisha mtu lakini aliweka bayana kwamba ngoma hiyo itatarajia kutoka  kati kati ya Februali mwaka huu, hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot