Jini Kabula bado yupo yupo kwanza - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday 8 February 2018

Jini Kabula bado yupo yupo kwanza



Miriam Jolwa maaru ‘Jini Kabula’

NA YUSUPH MWAMBA

MSANII mwenye uwezo mkubwa na ubunifu nchini, kwenye tasnia ya Bongo Muvi kutoka Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa maarufu kama ‘Jini Kabula’ amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuiigiza badala yake anajiwekeza kwenye ujasiriamali.

Kabula,ambaye hivi karibuni alizua taharuki baada ya kupatwa ugonjwa ambapo kwa sasa hali yake inakwenda vizuri na afya yake imeimarika.

Akizungumza na mwandishi Kabula, alisema sio kwamba ameachana na sanaa moja kwa moja lakini ameona akae pembeni ili kuangalia upepo mwingine ambako kwa sasa amejielekeza kwenye masuala ya ujasiriamali.

“Nipo poa kwa sasa namshukuru Mungu , afya yangu imeimarika, kikubwa kwa sasa nipo nje ya sanaa, lakini sijaiacha kabisa nafanya biashara zangu upepo ukikaa sawa nitarudi ila najua hakuna atakaechukua nafasi yangu kwakuwa kabula ni mbunifu na mtu makini katika kazi zake”, alisema

Msanii huyo, aliyewahi kutamba kupitia Tamthilia ya  Jumba la Dhahabu , yupo mbioni kuzindua nembo ya biashara  zake anazoziendesha japo hakutaka  kuziweka hadharani.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot