·
Hutibu, tezi dume, saratani, bawasiri
·
Vijana kuwa rijali, usichana
waliokoma hedhi
NA
ODRIANI NICOLAUS
WATU wengi mjini na
vijijini hupenda kupanda mti wa mzambarau kutokana na mti huo kuwa na kivuli
kizuri; ingawa kutokana na ongezeko la hitaji la mbao kila uchao wengine hupanda mti huo kwasababu hiyo.
Kwasababu ya kutofahamika sana kama mti dawa (medicinal
plant) ndiyo maana mzambarau hauvumi kwa sifa, japokuwa ni mti muhimu kiafya kutokana na dawa
zilizomo kwenye mti huo, kwa mujibu wa maelezo ya wataalamu wa afya.
Dk.
Elifariji Mtango, mtaalamu nguli wa sayansi ya mimea kutoka hopitali ya Chuo
Kikuu cha Kimataifa ya Tiba na Afya (IMTU)
cha Jijini Dar es Salaam, anasema majaribio ya tiba kwa wagonjwa kadhaa yanaonyesha
kuwa mizizi, magome na matunda ya mti huo husaidia tiba, kinga na lishe muhimu
kwa afya ya binadamu.
Anasema
Matunda ya mzambarau (zambarau) yana virutubisho vilivyomo kwenye mbegu za
tunda vinavyosaidia kuweka katika uzani sawa kiwango cha sukari mwilini. Wakati magome hutibu saratani za aina
mbalimbali na tezi dume kwa mizizi.
Akifafanua
kuhusu mizizi, Dk.Mtango anasema kama ilivyo tezi dume, mizizi ya mti huo iliyochimbwa, kusafishwa na
kukaushwa juani kisha kuchemshwa vizuri pia hutibu matatizo ya hedhi kwa wanawake
waliokoma hedhi kabla ya umri sahihi wa
ukomo.
Kama
haitoshi, maji hayo huongeza kinga mwili na nguvu za kiume kwa vijana na na
watu wanaume wengine wenye tatizo la kupungua nguvu za kiume, na tatizo la kuota kinyama
katika sehemu ya haja kubwa (bawasiri).
“Wapo
watu waliowapa tiba kwa mti huu na kupata matokeo mazuri, kutoka kwenye mateso
makubwa na sasa ni wenye furaha. Wanaendelea kufanya kazi zao bila matatizo
yoyote ikiwamo kurejesha heshima kwa ndoa ambazo zilikuwa mashakani kutokana
tatizo la nguvu za kiume, kuwaondoa katika gharama za tiba sukari na presha ambayo yamekuwa tatizo kwa
kizazi cha leo,”alisema.
Naye
mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho vya asili wa kituo cha Mandai Herbal
Clinick, Abdallah Mandai anasema kisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya
mfumo wa uyeyushwaji wa chakula ndani ya mwili. Ukosefu au upungufu wa kemikali
inayoitwa insulin husababisha ongezeko la kisukari inayojionesha kwa kiwango
kikubwa katika mkojo wa mwathirika.
Hata hivyo jamii inatakiwa kufahamu kuwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari hayalengi katika kuuponyesha ugonjwa, ila kumsaidia mgonjwa aweze kuishi maisha ya kwaida.
Matumizi ya zambarau huweza kumpa ahueni mgonjwa wa kisukari na kufafanua kuwa kinachopaswa kufanyika ni kukausha mbegu za zambarau, kisha kusaga mbegu hizo ili kupata unga laini.
Baada ya kufanya hivyo tumia nusu kijiko cha chai cha unga huo wa zambarau katika nusu glasi ya maji kila siku asubuhi kabla ya kula chakula chochote.
“Unaweza
pia kuchemsha majani mabishi (yale laini) na magome mabichi haya humkinga mtu
katika hatari ya kupata ugonjwa wa sukari hasa kwa wale ambao wameanzwa na
dalili… huweza kujikinga kwa kunywa
glasi moja yenye miligramu 200 hadi 350
na kunywa ujazo huo asubuhi kabla ya kula kituo chochote na jioni kadri
utakavyoshauriwa na mtaalamu,”alisema.
Kwa
mujibu wa mtaalamu huyo, juice hiyo husaidia mzunguko wa damu mwilini kutokana
na uwepo wa dawa katika majani hayo. Hiyo ni pampoja na dawa hizo kusafisha
taka kwenye mapafu ili kuruhusu oksijeni kupita vizuri na mtu kupumua ipasavyo.
No comments:
Post a Comment