Hussein Bakari: Kinda anayelilia namba Taifa Stars - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday 13 December 2017

Hussein Bakari: Kinda anayelilia namba Taifa Stars




NA ISSA RAMADHANI,
MCHEZAJI  wa timu ya Plaisance FC, Hussein Rashidi Bakari, anayekipiga katika timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza  nchini Seychelles,ametoa ushauri kwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars ,Salumu Mayanja , kuwapa nafasi wachezaji wa wanaocheza soka nje ya Nchi  ili kutoa changamoto kwa wachezaji wa ndani.

Miongoni mwa Timu alizowahi kuzitumikia hapa nchini kabla ya kwenda nje ya nchi ni pamoja na klabu ya Makumbusho FC inayoshiriki Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam na Simba Sc .

Mchezaji  huyo ambae ni zao la kituo  cha kukuzia vipaji kinachofahamika kwa jina la Makumbusho FC, ni mmoja wa vijana wanaoiwakilisha vyema nchi hii  na kupeperusha bendera ya Taifa letu katika na kuifanya kusomeka vizuri kwenye  ramani ya soka kama ilivyo kwa wachezaji waliotangulia Samatta, Ulimwengu pamoja na Saimoni Msuva.

Haussein alianza maisha yake ya soka akiwa na umri wa miaka kumi na nne {14} akikipiga kwenye kituo cha Soka cha Makumbusho,lakini alifanikiwa kupata nafasi kwende kuichezea simba{B} badaae alipandishwa kuichezea  simba ya wakubwa lakini akubahatika kupata nafasi katika kikosi cha kwanza .

Alikaa simba kwa kipindi cha miezi sita pamoja na kukosa kucheza kwa kipindi hicho lakini alibahatika kupata nafasi ya kufanya majalibio kwenye club ya Plaisance FC  ya nchini Seychelles timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini humo.

Katika majaribio, kijana huyo alifanikiwa kufaulu majaribio hayo , wakati anaendelea kukipiga kwenye timu ya Plaisance FC aliitwa kufanya majaribio  kwenye timu ya Foreshar FC ya ligi daraja la kwanza nchini Vietnam.

Katika kuonesha mapenzi yake kwa wachezaji, hapa nchini alionekana kuvutiwa sana na Mlinzi wa Klabu ya Soka ya Simba, Mohamed Hussein Zimbwe JR wakati ulaya akivutiwa sana na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Brazil na klabu ya PSG, Neymar JR.
Kwenye maisha hapakosi changamoto, mchezaji huyo alisema moja ya changamoto ambazo zilikuwa kikwazo kwake katika maisha yake ya  Soka ni ugumu wa maisha ulikuwepo kwenye Family yao ila haikumkatisha tama ya kwenda kufanya mazoezi akiwa ajapata ridhiki hivyo hakusita kutoa shukrani kubwa na pongezi za dhati kwa Kocha wake John Mashaka , Benchi la ufundi na  timu nzima ya Makumbusho FC, kwa ushirikiano mkubwa  waliompa katika kukabiliana na  changamoto alizozipitia .

Ushauri kwa Vijana wenzake wajitume kwa bidii wakiamini soka linahitaji uvumilivu na mipango thabiti, hivyo aliishauri Shirikisho la Soka la Tanzania (T.F.F) na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salumu Mayanja,  kuwapa nafasi wachezaji wanaochezea nje ya nchi ili kutoa changamoto.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot