Kero za wanawake zinazofanya upendo kupungua - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday 13 December 2017

Kero za wanawake zinazofanya upendo kupungua

Image result for mahusiano
Mahusiano'

NA ISSA RAMADHANI
KARIBU msomaji wangu katika safu ya mahusiano, ili tuweze kubadilishana mawazo na kuelimishama mambo mbalimbali yanayohusiana na masuala ya ndoa, uchumba, mafanikio na changamoto zake.
Leo tutazungumzia kero zinazofanywa na wanawake ambazo zinawakera waume zao katika ndoa. 
KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI
Tabia  ya mke kutoka na kurudi nyumbani akiwa amechelewa mno au usiku tena wakati mwingine bila kutoa taarifa kwa mumewe inakera wanaume wengi. 

KUFANYA MAPENZI NJE YA NDOA
Mume anapoona nyendo za mkewe hazieleweki anakuwa mkali sana na na kusababisha mgogoro ndani ya nyumba na wakati  mwingine husababisha mume kutofanya tendo la ndoa na mkewe kwa kuhofia kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Mapenzi hupungua kwa kiasi kikubwa na uaminifu kwa mkewe unakuwa haupo tena..
KUWA NA MARAFIKI WABAYA
 Katika  ndoa mwanaume hapendi kuona mkewe ana marafiki wanawake wenye mienendo mibaya, mfano malaya, wakorofi na wanaopeenda kutoka ‘out’ kila wiki kwa wa kuhofia kuambukizwa tabia mbaya, usaliti na kusahau majukumu ya kulea familia na kumuhudumia mume.
 KUPENDELEA WAZAZI WA UPANDE MMOJA
Mwanamke anayewajali zaidi wazazi wake pekee kuliko wa mumewe, hata ndugu wanapaokuja upande wa mumewe  hapendi ni tabia inayowakera wanaume wengi. Tabia hii ikiendekezwa husababisha hata watoto  na husabisha  mtafaruku katika familia.

KUTOA SIRI ZA NDANI NJE
Wapo baadhi ya  wanawake wanatoa mambo yao ya ndani  kwa mashoga zao bila kujali. Aidha kugawa vitu nje bila mpangilio na kusahau majukumu ya nyumbani ni kero kwa mume.

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA
 Baadhi ya wanawake hutumia fedha za matumizi ya familia bila utaratibu na hawazingatii bajeti na wa wakati mwingine hukataa fedha za matumizi  anazopewa kwa kisingizio kuwa hazitoshi hata pale anapoona hali ya mumewe kwa wakati huo si nzuri kifedha lakini hapo upande wa pili unakuta mwanamke huyohuyo anatumia gharama kubwa kujipamba na kufurahisha marafiki. Pia tabia ya uongo  na umbea huchukiza  wanaume wengi kwa wake zao.

KUTOMJALI  MUME
Baadhi ya wake hujisahau katika kumjali mume, kwa mfano kunyooshea nguo pasi, kumchagulia nguo ya kuzaa, kumuwekea maji ya kuoga  na kula naye chakula pamoja na kutoshukuru mume akimletea zawadi. Pia tabia ya kuwaachia kazi zote za ndani madada za kazi hata zile apasazo mke kumfanyia mumewe hukera wanaume wengi na wakati mwingine husababisha mume kuanza mahusiano ya kimapenzi na dada wa kazi.
KUFICHA MAOVU YA WATOTO
Wapo baadhi ya kina mama wanaficha maovu ya watoto wao hasa mabinti ili baba asimudhibu mtoto au kukemea. Hili linakera sana wanaume kwani hawapendi tabia hizo na wakati mwingine hupunguza mapenzi kwa mkewe.

KUTOOMBA MSAMAA
Baadhi ya wanawake wanatabia ya kutoomba msamaha kwa waume zao wanapokosea. Wengine huwa na tabia ya kufyonza, kutoitika wakiitwa, kukataa kutembea au kukaa pamoja  kujadili masuala ya maendeleo na familia kwa ujumla na kutamani kuwa na maisha ya juu kuliko uwezo wa mume.

USHAURI
Wanandoa wanapaswa kuwa makini katika maisha yao na uzingata  misingi ya ndoa. Aidha, wanatakiwa kuheshimiana, kuepuka kauli tata, kupendana, kusaidiana na kujadili kwa staha tofauti ili kuwa ndoa yenye furaha na familia bora ya watoto wenye afya na akili njema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot