Jinsi ya kujinasua msongo wa mawazo - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday 13 December 2017

Jinsi ya kujinasua msongo wa mawazo

Image result for mawazo
SAIKOLOJIA
NA ISSA RAMADHANI
NI jambo la kumshukuru Mungu kukutana tena katia safu hii ya saikolojia na mahusiano. Leo tutazungumzia tatizo la msongo wa mawazo na namna ya kuondokana nalo.
Mara nyingi katika jamii au familia zetu tumekuwa tukishuhudia watu wengi wakisumbuliwa na msongo wa mawazo kwa kujua au kutojua na tatizo hili  limekuwa lilikuwa kwa kasi.
Tafiti zimeonesha tatizo la msongo wa mawazo likizidi husababisha mtu kuugua ugonjwa wa akili na kuingia gharama kubwa katika  matibabu.
Hata hivyo zipo njia mbalimbali ambazo mtu anayekumbana na hali hii anaweza kuzitumia ili kuondokana nalo.

KUZUNGUMZA NA WATU
Wataalamu wa saikolojia wanasema kuzungumza na watu ni njia mojawapo ya kuondoa  tatizo la msongo wa mawazo, Wanasema mtu anapoficha tatizo linalomsumbua mawazo husongamana kwani yanakuwa yamekosa pakutokea hivyo kusababisha matatizo ya kiafya hasa akili. Kiafya binadamu anapaswa kuongea na kusilizwa anapokumbana na tatizo ambalo mwenyewe limemshinda kulitatua. Kwa kawaida mwanamke anapaswa kuzungumza maneno 24000 na mwanamume maneno 6000 kwa siku ili aweze kuwa wa kawaida.

KUWA NA MUDA WA KUFURAHI
Kitendo cha kuwa na furaha hutibu tatizo la msongo wa mawazo. Wataalamu wa saikolojia wanasema kucheka kunaongeza afya na siku za kuishi, mfano nchi zilizoendelea kama Marekani kuna maeneo maalumu yamejengwa watu wanaenda kuangalia vichekesho na kucheka ili kuwaondolea msongo wa mawazo. Kwa ufupi kucheka na kufurahi ni tiba na ni afya.

KUWA NA MUDA WA KUTOA MACHOZI
Hili jambo wanasikolojia wanashauri unapopata muda wa kulia fanya hivyo na usijizuie na inapobidi jiachie kulia hasa machozi yatoke kwa wingi.  Kwa bahati mbaya mila za Kiafrika   suala la kutoa machozi inachukuliwa  ni udhaifu au utoto kwa mwanaume lakiniu katika sayansi kulia ni tiba. Wanasaikolojia wanasema machozi yanasaidia kuondoa sumu mwilini na yanapotoka husaidia kuondoa bacteria  na kufanya mtu kujisikia vizuri. 

FANYA KAZI UNAZOPENDA   
Jitahidi kufanya jambo unalolipenda na kukupa faraja,  mfano  kuangalia filamu, kuogelea, kusoma vitabu,  kucheza mpira na mengineyo, hali hiyo itakusaidia kuondokana na msongo wa mawazo.. 

JICHANGANYE NA WATU
Ni vizuri ukajichanganya  katika shughuli mbalimbali, mfano sherehe, usafi,  mikutano, mijadala,  misiba na matamasha ya muziki. Huko utajikuta ukizungumaza na kujadili mambo mbalimbali na kujifunza changamoto ambazo watu wengine wanazipitia na kuondokana nazo.   

KUWA NA MUDA WA KUPUMZIKA
. Ukiwa nyumbani hakikisha unapata muda wa kutosha kupumzisha mwili na kulala na hakikisha unakula vyakula vya  kujenga mwilini na akili.

PENDEZESHA CHUMBA UNACHO LALA
Si sebuleni pekee panatakiwa papendendeze bali  na chumba unacholala  kinapaswa kiwe safi, kuvutia  kwa kupanga vitu vizuri na kuwa na hewa safi ya kutosha Unapaswa kusafisha mashuka ya kitanda na kujifunika, godoro zuri, kudeki chumba na kiwe na mwanga wa kutosha .
Wataalamu wa masuala ya saikolojia na afya wanasema nusu ya maisha yako  unatumia chumbani unakolala. Usiku lala kwa muda usiopungua saa saba ili kuondokana na tatizo la msongo wa mawazo. 

FANYA MAZOEZI
Jitaidi kufanya mazoezi mara kwa mara angalau dakika 30 kila siku. Mazoezi si tu tiba ya msongo wa mawaz, bali pia hata kisukari na moyo na kuboresha ufanisi wa mwilini.  

SHUGULIKIA TATIZO
Kama ukiona tatizo haliondoki ni vyema ukawaona watu wa ushauri nasaha na wanasiaklojia ili kuona nama ya kuondokana na tatizo la msongo wa mawazo na mengineyo




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot