Kijana Mussa Shingano ambaye ni mlemavu wa mguu anayejishughulisha
na shughuli za ujasiriamali wa kuunga na
kuchomea vifaa mbalimbali vya chuma akiwa katika moja ya vitanda anavyotengeneza
, ofisini kwake eneo la Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam. (PICHANI)
|
Na Mohamed Ng’oula
KATIKA kwenda sambamba na mikakati ya nchi ya Tanzania ya viwanda, vijana wengi sasa
wamekuwa wakichangamkia fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo
kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Harakati hizo zimewasukuma vijana
wengi hata wenye ulemavu wa viungo kuacha kuombaomba na
kujishughulisha katika shughuli za maendeleo.
Kwa bahati mbaya sana kuna baadhi ya
vijana hususan wenye ulemavu bado wanajitenga katika
kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujiona wao ni tofauti na watu
wengine jambo linalo sababisha ongezeko la ombaomba nchini.
Hata hivyo, hali ni tofauti kwa kijana
mlemavu, Mussa Shingano, ambaye katika kupambana na umasikini ameamua kupambana
na hali yake hadi kufikia kuwa fundi wa kuchomea vifaa mbalimbali vya chuma.
Safu hii ya Tuishivyo, imemtembelea
kijana huyo mwenye ulemavu wa miguu nyumbani kwake Gongo la Mboto, jijini Dar
es salaam na kuzungumza nae masuala mbalimbali kuhusu harakati za maisha na
namna anavyokabiliana na changamoto mbalimbali.
Shingano anaeleza pamoja
na hali aliyonayo hakuwahi kujiona yupo tofauti na binadamu wengine na anachofikilia ni
kufanya kazi kwa bidii ili afanikiwe katika maisha yake.
Kijana huyu aliyezaliwa mwaka
1992 mkoani Tanga, wilaya ya Pangani, katika kijiji cha Bushili anasimulia
tangu alipozaliwa alipata ulemavu wa miguu yote miwili na jitihada mbalimbali
za kumrudisha katika hali ya kawaida zilishindikana na kujikuta
akiwa alivyo hadi sasa.
“Nilizaliwa nikiwa mlemavu lakini
kutokana na upendo wa mama yangu nilijiona mimi ni sawa na watu wengine, jamii
haikunitenga mpaka ikafika wakati nikamuomba mama anipeleke shule kwani nilitamani kusoma nilipowaona wenzangu wakienda
shule,” anasema Singano.
HARAKATI ZA MAISHA
Anasema mwaka 2000 alianza darasa la
kwanza katika Shule ya Msingi Funguni na kumaliza elimu ya msingi 2007 na mwaka
uliofuata alijiunga na elimu ya sekondari hapohapo Funguni na kuhitimu kidato
cha nne 2011 ingawa hakubahatika kuendelea na masomo kutokana na matokeo yake hayakuridhisha.
“Sikukata tamaa baada ya kushindwa
kuendelea na masomo nikamuomba mama yangu pamoja na majirani zangu msaada wa
kwenda kusomea ufundi jijini Dar es Salam, niliomba mpaka ustawi wa jamii
nikasaidiwa kusomeshwa ufundi wa kuunganisha vyuma chakavu,” anasema Shingano.
MAISHA JIJINI
DAR ES SALAAM
Anasimulia kuwa, pamoja na ulemavu
alionao na umasikini wa familia yake hakutaka kuwa kuwa tegemezi au ombaomba kama
walivyo baadhi ya watu wenye ulemavu.
Anasema alianza kusomea ufundi
katika chuo cha ufundi cha watu wenye mahitaji maalumu kilichopo Yombo, jijini
Dar es Salaam kwa muda wa miaka miwili akahitimu na kuanza kujishughurisha
katika ujuzi wake huo mpaka hivi sasa.
“Nimemaliza elimu ya ufundi baada ya kuomba
michango kwa watu mbalimbali na sasa nina ofisi yangu ya kuchomea
mageti, vitanda vya chuma na vifaa vya chuma maeneo ya Mombasa huko Gongo
la Mboto, ingawa vifaa havijatimia lakini sio sawa na kuombaomba,” anasema.
CHNGA
MOTO ZA MAISHA
Kama unavyo jua kila jambo lina
changamoto zake, Singano anasimulia kuwa, tangu afariki baba yake mzazi akiwa
darasa la kwanza, yeye alishikilia jukumu la kuwa kiongozi wa familia,
hivyo wakati yupo shule anasoma pia alikuwa akimuhudumia mama yake mahitaji
mbalimbali kutokana na uzee alionao jukumu ambalo anaendelea nalo mpaka
hivi sasa.
Hata hivyo, anasema pamoja na kufungua
ofisi yake, vifaa alivyonavyo havikidhi mahitaji yake katika suala zima la
kiufundi hali ambayo imekuwa ikimkwamisha kufanya kazi zake.
WITO
Pia amewaomba wananchi wenye ulemavu
kama yeye na wasio na ulemavu kuacha kubweteka na badala yake wachangamkie fursa
mbalimbali zinazotolewa na serikali katika viwanda na pia wajiajiri badala ya
kukaa nyumbani na kukata tamaa.
“Ni waombe walemavu wenzangu
na wasio walemavu kuacha kubweteka wajitume; kama mimi naweza kwanini wewe ushindwe pia
niwakaribishe watu mbalimbali wenye ujuzi hususan walemavu waje katika ofisi
yangu tushirikiane kazi ili tujenge uchumi wa taifa letu, najisikia vibaya
nikiwaona vijana hawafanyikazi wanaombaomba, ifike wakati tuache kuombaomba,”
anasema Singano.
No comments:
Post a Comment