![]() |
LONDON,England
wa Misri amechaguliwa
kuwa mshindi wa Tuzo ya BBC kwa Mwanakandanda Bora wa Afrika Mwaka 2017. (pichani)
Nyota huyu wa Liverpool alipata kura
nyingi zaidi ya Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Naby Keïta wa Guinea, Sadio
Mané wa Senegal na mchezaji wa Nigeria Victor Moses.
"Nimefurahi sana kupata tuzo
hii," mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliiambia BBC Sport.
"Huwa ni hisia ya kipekee
unaposhinda kitu. Unahisi ulikuwa na mwaka mzuri sana. Kwa hivyo nina furaha
sana. Ningependa kushinda tena mwaka ujao!"
Salah, aliyefunga mabao mengi zaidi
ligi kuu England, akiwa na mabao 13, amekuwa na mwaka wenye mafanikio.
Mapema 2017 alikuwa nyota wa Misri
walipochukua nafasi ya pili katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Baadaye mwakani, mshambuliaji huyu
aliye na kasi alichangia katika magoli yote yaliyowasaidia Mafirauni kufuzu
kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1990 -
aliwasaidia wenzake kufunga mabao mawili, naye akafunga mabao matano, moja
ikiwa penalti kati yao na Congo iliyowawezesha kufuzu kwa fainali hizo za
Urusi.
"Ninataka kuwa mwanakandanda
bora zaidi wa Misri kwa hivyo mimi hutia bidii," anasema kijana huyu
ambaye amekuwa raia wa tatu wa Misri kupata tuzo hii tangu 2008.
"Mimi hufuata njia yangu na
ninataka watu wote Misri kufuata njia yangu"
Mchezo wake kwenye klabu yake
umekuwa mzuri sana, sawa na ule wa nchi yake.
Nchini Italia, alifunga mabao 15 na
kusaidia ufungaji wa mengine 11 na kuisaidia Roma kumaliza katika nafasi ya
pili kwenye Serie A, nafasi yao bora zaidi kwenye ligi katika miaka saba, kabla
ya kujiunga na Liverpool na kufunga bao mara 13 katika mechi zao 16 za kwanza
kwenye ligi.
"Ningependa kuwashukuru
wenzangu wa timu ya Liverpool na pia nilikuwa na msimu mzuri na Roma, kwa hivyo
lazima niwashukuru wenzangu huko na wale pia wa timu ya taifa," alisema
Salah.
"Tangu nije hapa, nilitaka
kujia bidii sana na kuonyesha kila mtu uchezaji wangu. Nilitaka kurudi Ligi ya
Premia tangu nilipoondoka, kwa hivyo nina furaha sana."
Salah amerejea Ligi ya Premia kwa
kishindi msimu huu, tofauti sana na alipokuwa kwenye ligi hiyo mara ya kwanza
akiwa na Chelsea kati ya 2014-15.
"Anastahiki," anasema
meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, aliyemkabidhi mchezaji huyo tuzo yenyewe
katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Melwood.
"Kwa kweli mimi ni mtu mwenye
bahati sana. Nilikuwa na fursa ya kufanya kazi na wachezaji wachache wa kipekee,
wazuri, na nina furaha kwamba sasa nina Mo.
"Jambo zuri ni kwamba yeye bado
mdogo wa umri, anaweza kuimarika sana, ana uwezo mwingi ambao bado tunaweza
kuufanyia kazi, na hivyo ndivyo inafaa kuwa. Ni furaha sana kwangu, kusema
kweli, kufanya kazi naye."
Salah sasa ameongeza jina lake
kwenye orodha ya wachezaji hodari kutoka Afrika, kama vile Abedi Pele, George
Weah, Jay-Jay Okocha na Didier Drogba, ambao wamewahi kushinda Tuzo ya BBC kwa
Mwanakandanda Bora wa Afrika wa mwaka.
"Nina furaha isiyo na kifani
kuwa kama wao katika kushinda tuzo hii," amesema raia huyo wa Misri,
ambaye amewafuata raia wenzake Mohamed Barakat (2005) na Aboutreika (2008)
katika kushinda taji hilo.
Washindi wa awali wa Tuzo ya BBC kwa
Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka:
2016: Riyad Mahrez (Leicester City
& Algeria)
2015: Yaya Toure (Manchester City
& Ivory Coast)
2014: Yacine Brahimi (Porto &
Algeria)
2013: Yaya Toure (Manchester City
& Ivory Coast)
2012: Chris Katongo (Henan
Construction & Zambia)
2011: Andre Ayew (Marseille &
Ghana)
всексти пелиния - Titsanium-Arts
ReplyDeleteвсексти пелиния - бателиния edc titanium - лииекки велиния сплания thaitanium катки по незена. burnt titanium в titanium sunglasses велиния катки titanium vs ceramic по незена дать.